Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, April 28, 2014

WLADIMIR KLITSCHKO AMTWANGA LEAPAI KAMA GUNIA NA KUTETEA MATAJI YAKE


BONDIA Wladimir Klitschko ameendeleza ubabe wake katika ndondi za uzito wa juu baada ya usiku wa kuamkia leo kumchapa kwa Knockout (KO) ya raundi ya tano, Alex Leapai katika pambano la kutetea mataji yake. 
Klitschko, alitumia mikono yake mirefu kumchapa kama 'mwanawe' mpinzani huyo wa Samoa mzaliwa wa Australia, ambaye raundi ya tano alisalimu amri katika pambano lililofanyika mjini Oberhausen, Ujerumani Magharibi. 
Leapai alikwenda chini baada ya kuchanganyiwa makonde ya mikono yote, kushoto naa kulia mfululizo. 
Aliinuka kujaribu kutaka kuendelea, lakini kwa nia nzuri, Klitschko raia wa Ukraine akajisogeza mbali zikiwa zimesalia sekunde 58 raundi hiyo kumalizika.
Pokea hiyo: Konde la Klitschko likichapa kidevu cha Leapai jana katika pambano la ubingwa wa dunia uzito wa juu mjini Oberhausen, Ujerumani Magharibi.
Down you go: Klitschko watches as Leapai falls to the canvas
Chini: Klitschko akimuangalia mpinzani wake, Leapai anavyopambana na sakafu
Conveyor belt of success: Wladimir Klitschko celebrates victory over Australia's Alex Leapai after the WBA, IBF, WBO and IBO title bout
Mataji kibao: Wladimir Klitschko akisherehekea ushindi wake dhidi ya Alex Leapai ambao umemfanya atetee mataji yake ya WBA, IBF, WBO na IBO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...