Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, April 17, 2014

MSAMA PROMOTIONS YATANGAZA VITUO VYA KUUZIA TIKETI ZA TAMASHA LA PASAKA


 KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka imetangaza vituo vitakavyouzwa tiketi kwa ajili ya tamasha hilo kwa mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama tiketi hizo zitauzwa katika vituo vitano kwa lengo la kupunguza usumbufu kwa mashabiki wenye nia ya kushiriki tamasha hilo.

Msama alitaja vituo vitakavyouzwa tiketi hizo ni pamoja na Puma Mwenge na Uwanja wa Ndege, Best Bite Namanga, BM Kinondoni  na ofisi za Msama Promotions Kinondoni.Aidha Msama alitoa wito kwa waumini na wadau mbalimbali wa tamasha hilo kujitokeza kwa wingi kujipatia tiketi ambazo zitafanikisha kuhudhuria.

Msama aliweka bayana viingilio ni shilingi 20,000 kwa viti maalum, VIP ni shilingi 10,000, kawaida ni shilingi 5000 na watoto ni shilingi 2000.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...