Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, April 13, 2014

Nani wa kumzuia Tambwe asitwae kiatu cha Dhahabu?


Amissi Tambwe
Na Rahim Junior
AMISSI Tambwe anacheeka! Kufuatia kushuhudia washambuliaji wa timu pinzani katika Ligi Kuu Tanzania Bara wakishindwa kumfikia kileleni kwenye orodha ya Ufungaji Bora licha ya kutoshuka dimbani katika mechi kadhaa kutokana na majeruhi aliyonayo.
Rais huyo wa Burundi anaongoza mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu akiwa na magoli 19, sita zaidi na ya Mfungaji Bora wa msimu wa mwaka jana, Kipre Tchetche anayemfukizia kwenye nafasi ya pili akiwa na mabao 13.
Tambwe aliyenyakuliwa na Simba msimu huu akitokea Vital'O, baada ya kunyakua kiatu cha Dhahabu cha Kombe la Kagame, amewaacha mbali pia nyota wa Yanga wanaofuatia katika orodha hiyo ya ufungaji bora.
Mrisho Ngassa aliyefunga hat trick wiki iliyopita Yanga ilipoizamisha JKT Ruvu pamoja na Hamis Kiiza 'Diego' wana mabao 12 kila mmoja, huku mchezaji aliyeshika nafasi ya pili msimu uliopita Didier Kavumbagu akiwa na magoli 11 sawa na Elias Maguli na ligi ikielekea mwisho.
Kuna kila dalili kwamba Tambwe atanyakua kiatu hicho, labda tu itokee miujiza kwa akina Kipre Tchetche, Ngassa, Kiiza na Kavumbagu wafunge kapu na mabao katika mechi za raundi mbili zilizosalia zikiwemo za leo na zile za kufungia msimu Jumamosi ijayo.
Wafungaji Bora:
19- Tambwe Amisi (Simba)
13- Kipre Tchetche (Azam),
12- Mrisho Ngassa, Hamis Kiiza (Yanga),
11- Didier Kavumbagu (Yanga), Elias Maguri (Ruvu Shooting)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...