Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 31, 2012

MPAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare

SUPER D BOXING COACH AKIMWELEKEZA KING CLASS MAWE
Mabondia Hassan Mandulla na Jems Martin wanatarajia kupanda ulingoni Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare Dar es salaam akizungumza mpambano huo mwandaaji Waziri Rosta
amesema kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo ya mabondia maarufu na chipkizi alisema mapambano ya utangulizi ni Fadhiri Majia na Anton Matiasi mpambano mwingine

Utawakutanisha Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma na Chaeles Mashali atavaana na Adam Ngange, Julias Noro atapambana na Abdallah Luwajempambano mwingine utawakutanisha Rajabu Tumaini na Daudi Anton na Rashid Mohamed Atavaana na Eliman Richard wakati Rashid Hamisi atamvaa Omary Shabani

Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.

 michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.


 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 

 
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

KUZIMWA KWA MITAMBO YA ANALOJIA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO JANUARY MAKAMBA ATOA TAARIFA KWA UMMA.


Ndugu Wananchi,
 Mtakumbuka kuwa hapo tarehe 23 Februari 2012 tuliwatangazia kupitia vyombo vya habari juu ya usitishwaji wa matangazo ya televisheni kwa kutumia teknolojia ya analojia kwenda katika mfumo mpya unaotumia teknolojia ya dijitali.
Napenda kuwaleleza kuwa, maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia kuanzia tarehe 31 Desemba 2012 yamekamilika kwa mujibu wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo, napenda sasa kutoa taarifa kuwa uzimaji wa mitambo ya analojia utafanyika kwa awamu kama ifuatavyo:-
    (1) Dar Es Salaam-31 Desemba, 2012;
    (2) Dodoma & Tanga- 31 Januari, 2013;
    (3) Mwanza-28 Februari, 2013;
    (4) Moshi & Arusha-31 Machi, 2013;
    (5) Mbeya-30 Aprili, 2013.
 Tumeamua kuanza kuzima mitambo hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam kwanza ili kutoa fursa kwa makampuni yenye leseni kusimika mitambo ya utangazaji wa dijitali katika mikoa mingine. Makampuni haya yamejipanga kukamilisha usimikaji wa mitambo hiyo katika mikoa minane katika miezi minane ijayo.
Mitambo ya analojia itakayozimwa kesho ni ile iliyopo Kisarawe na Makongo. Vituo ambavyo siku ya tarehe 1 Januari 2013, vitapaswa kuanza kutangaza matangazo kwa mfumo wa dijitali ni TBC1, ITV, EATV, Channel 10, StarTV, DTV, CapitalTV, TumainiTV, ATN, MlimaniTV, C2C, CTN, CloudsTV na Efatha.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inafanya jitihada za kutosha kuhakikisha kwamba makampuni yenye leseni za kusambaza ving’amuzi yanakuwa na ving’amuzi vya kutosha na vingine vimeagizwa ili kukidhi mahitaji ya baadaye na vile vilivyopo sokoni vina ubora unaokubalika.
Vilevile, Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itahakikisha kwamba zoezi la uhamaji linafanyika bila usumbufu na kero kwa wananchi. Makampuni yanayouza ving’amuzi yameagizwa yaimarishe huduma kwa wateja wakati wa kuuza ving’amuzi na hata baada ya ununuzi iwapo wananchi watakuwa na matatizo na ving’amuzi.
  
Zoezi hili la uhamaji ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Tutakapokuwa tumekamilisha uhamaji, huduma za mawasiliano na utangazaji zitapanuka na kuwa bora zaidi. Kwa mfano, itawezekana sasa kuangalia televisheni kupitia simu zetu za mikononi. Vilevile, itawezekana, kwa bei nafuu kabisa, kwa mtu mwenye uwezo wa kutengeneza vipindi kukodisha chaneli yake na kutangaza vipindi vyake. Vilevile, bei za mawasiliano na utangazaji zitashuka, na tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye mapinduzi ya teknolojia duniani, ambayo nchi yetu haiwezi kubaki nyuma.
Ndugu Wananchi,
Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhamaji huu. Serikali inatarajia kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji na wananchi kwa ujumla katika kipindi cha uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni ili kufanikisha zoezi la uzimaji wa mitambo ya utangazaji ya teknolojia ya analojia.
Uhamaji huu hautahusu televisheni za wananchi zinazopata matangazo kupitia madishi (nyungo) (satellite) au nyaya (cables). Hivyo, wananchi wanaopata matangazo kupitia DStv, Zuku, na nyinginezo wataendelea kupata matangazo yao kama kawaida.
Ndugu Wananchi
Kama kuna mwananchi yoyote ana kero, malalamiko, swali au anahitaji maelekezo kuhusu uhamaji, awasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia namba 0784-558270; 0784558271 au barua pepe: malalamiko@tcra.go.tz
  
Ndugu Wananchi,
Nawashukuru kwa kunisikiliza.

"NAFSI NI NYONGE" TUSAMEHEANE NA MAISHA YAENDELEE. KARIBU 2013 KWA UFANISI ZAIDI


Wapendwa ndugu, jamaa na marafiki popote pale mlipo,yamebaki masaa kadhaa kuuaga mwaka 2012, ambao kwa hakika ulikuwa na changamoto nyingi za kimaisha, dhoruba za hapa na pale wengi zilitukumba, lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu akatushika mkono akatuinua na maisha yakaendelea.

Binafsi mpaka dakika hii namshukuru Mungu nikiwa mwenye afya njema kabisa. Maisha ya sasa Wanadamu wengi wamekuwa dhaifu kwa mambo mengi, lakini Mungu ndiyo njia sahihi wa kumtumia katika sala zako kuyashinda majaribu na madhaifu ya Dunia. Yako mengi ambayo naweza nikayaandika hapa lakini bado yasitoshe pia. Nasema asanteni kwa ushirikiano wenu mkubwa kwa namna moja ama nyingine, kama kuna mahali nilikosea, tukakwaruzana kidogo basi "NAFSI NI NYONGE" Tusameheane na maisha yaendelee.

Tunahamia mwaka mwingine mpya kabisa 2013, basi na tuendelee na ushirikiano huu tuliokuwa nao kwa mambo mbalimbali yenye kujenga na kuleta tija katika maisha yetu, Mwaka 2013 uwe wa kuhakikisha kweli sote pia tumehamia kwenye mfumo wa kidijitali, tushauriane, tuelemishane tunyooshane njia iliyo sahihi ili kila mmoja kila wakati abaki nafsini mwake mwenye furaha daima, Pia tumtangulize Mungu kila wakati kwa kila jambo ili pia azidi kuzibariki kazi za mikono yetu daima.

Kwa Blogaz wenzangu, changamoto nyingi tumekumbana nazo 2012, ikiwemo tatizo kuu la KUKOPY NA KUPASTE.! Na nyinginezo nyingi tuzijuazo zinatusumbua kwa namna moja ama nyingine, basi ni nyema 2013 iwe ya kuzitafutia ufumbuzi, kama si kuzimaliza kabisa basi angalau tuendelee kuzipunguza ili kuzimaliza kabisa, huku suala la kujituma na ubunifu vikiwa ndio ngao kuu ya mabadiliko miongoni mwetu. Ushirikiano tuliokuwa nao umeonesha tuna uwezo mkubwa wa kuisadia jamii inayotuzunguka na hata serikali pia kwa namna moja ama nyingi, basi tusimame kidete kuhakikisha ushirikiano huu hauteteleki ama haupotei kirahisi, badala yake tuiimarishe zaidi kila kona.

Natoa shukurani za dhati kabisa kwa makampuni na wadau mbalimbali ambayo/ambao kiukweli yametoa mchango mkubwa kuhakikisha tunasonga mbele na libeneke hili , si vibaya nikiyataja makampuni hayo kuwa ni Serengeti Breweries Ltd, Airtel, Bayport, Msama Promotions Ltd, kampuni ya R&R, Dada Teddy Mapunda, Hoyce Temu, Blogaz wote (bila kinyongo) na wengine waliotupa hatua ya kusogea kwa namna moja ama nyingine, Mungu awabariki sana.

Asanteni 
Nawatakia heri ya sikukuu ya Mwaka mpya.

NI USIKU WA ZAWADI MWAKA MPYA NDANI YA DAR LIVE


JK KUTOA SALAMU ZA MWAKA MPYA


                                                                     Rais Jakaya Kikwete

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, jioni ya leo, Jumatatu, Desemba 31, 2012, atatoa salamu maalum za Mwaka Mpya kwa wananchi.
Rais Kikwete atatoa salamu hizo kupitia hotuba yake kwa Taifa ambayo ataitoa kwa njia ya redio na televisheni.
Katika salamu hizo, Rais Kikwete anatarajia kuzungumzia masuala mbali mbali kuhusu matukio makubwa ya mwaka huu na mengine muhimu yaliyojitokeza katika jamii ya Tanzania katika miezi 12 iliyopita.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
31 Desemba, 2012

MASHAHIDI WAKWAMISHA KESI YA PONDA LEO


 Katibu Mkuu  wa  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo pamoja na washtakiwa wenzake 49, hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa kutokana na mashahidi upande wa mashtaka kutofika mahakamani hapo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Katibu Mkuu  wa  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa na mshtakiwa mwenzake,  Mukadam Abdal Swalehe (kushoto)
 Baadhi ya wafuasi wa Sheikh Ponda wakiwa katika viunga vya mahakama ya Kisutu
Katibu Mkuu  wa  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na mshtakiwa mwenzake Mukadam Abdal Swalehe wakitoka mahakamani chini ya ulinzi wa askari magereza.
 Ulinzi uliimarishwa katika eneo la Mahakama ya Kisutu leo.
 Katibu Mkuu  wa  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na washtakiwa wenzake. 

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKABIDHI ZAWADI ZA MWAKA MPYA KWA KITUO CHA TUSHIKAMANE CHILDREN CARE TRUST FUND.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akikabidhi Mbuzi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tushikamane Children Care Trust Fund Bw. Gratho Messy Mbele (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Shule ya Tushikamane Bi. Euphrosine Mtundu, kama zawadi kwa watoto yatima wa kituo hicho ambapo panapo majaliwa hapo kesho atajumuika nao kupata chakula cha mchana. Anayeshuhudia tukio hilo ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi (wa pili kushoto)

Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa kituo hicho chenye lengo la kuhudumia watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile elimu, afya, chakula, malazi, mahitaji ya shule, pamoja na huduma za kisaikolojia na ulinzi dhidi ya manyanyaso.

Viongozi wa kituo hicho wakimshukuru Mstahiki Meya Jerry Silaa.

Meya wa Manispaa Mstahiki Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi zawadi za vyakula ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao katika kusherehekea mwaka mpya 2012/2013.
Kila mwaka wakati wa sherehe za mwaka mpya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala yeye binafsi hutoa sadaka kwa wahitaji kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza mwaka salama.
Leo Mstahiki Meya Jerry Silaa ametoa chakula kwa kituo cha Watoto Yatima na watoto Yatima na watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi cha Tushikamane Children’s Care Trust Fund ambapo pamanapo majaliwa hapo kesho atakula chakula pamoja nao.
Asasi hiyo ya Tushikamane Children’s Care Trust Fund ilianzishwa mwaka 2001 na kupata usajili wa kudumu mwaka huo huo ili iweze kujiendesha kwa mujibu wa sheria za nchi.

YANGA YAANZA MAZOEZI RASMI UTURUKI.


Tumeanaza mafunzo!
Tunadaka kwa utaratibu.

YOUNG Africans Sports Club imeanza mazoezi leo asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.
Mji wa Antalya ni maarufu katiak medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameandaa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huo watasherehekea pamoja.

TRA Tatizo nini Sheria au Mfumo?


Kwamujibu wa sheria tunazotangaziwa na mamlaka ya mapato hapa nchini mwenye bango hili hapa nae anapasa kulilipia kodi lakini je niwenye mabango wangapi kama haya wanalipa? nakama wanalipa hiyo kodi kweli inafika TRA ? Kama halipi au kodi haifiki tatizo nini Sheria au mfumo? Tushirikiane tujenge nchi! Bango hili limenaswa na kamera yetu mbele ya kituo cha Polisi cha Urafiki hii leo. Kama kungekuwa na umakini wa ukusanyaji wa kodi kutokana na vyanzo vilivyoainishwa na sheria serikali ingeweza kukusanya kodi ya karibu Tsh.Trilioni moja kwa mwezi badala ya i Tsh Billioni500 za sasa.

SALAAM ZA MWAKA MPYA.


MTU MMOJA AJERUHIWA MADARASA SITA YAEZULIWA NA UPEPO.


Madarasa ya shule ya sekondari mnacho yaliyoezuliwa na upepo mkali uliovuma jana kwenye baadhi ya Vijiji Wilayani Ruangwa na kusababisha watu kadhaa kukosa mahala pa kuishi na kusababisha watu wengine kujeruhiwa pamoja na madarasa hayo sita kuezuliwa mapaa.
Bati zilizoezuliwa na upope huo mkali ulioacha athari kubwa.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Reubern Mfune Akitoa taarifa ya maafa hayo ya jana katika kikao cha  Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ruangwa  kwenye kikao kilichofanyika leo. Picha na Ahmed Abdullazizi-Lindi.

ONYESHO LA BENDI YA AKUDO IMPACT MSASANI BEACH


 Wanenguaji wa bendi ya Akudo Impact, wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao, lililofanyika jana jumapili kwenye Ukumbi wa Msasani Beach Club, ambapo bendi hiyo hufanya onyesho la Bonanza katika ukumbi huo kila siku ya Jumapili.
 Mashambulizi yanaendelea jukwaani,,,
Rapa wa bendi hiyo (kulia) akiwachezesha wanenguaji wa bendi hiyo wakati wa onyesha hilo.

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI


Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na makazi.

 Bango linaloonyesha Idadi ya watu wote Watanzania, baada ya kuhesabiwa katika zoezi la kuhesabu Sensa lililoanza mwezi Agosti mwaka huu na kufikia tamati hii leo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, alipotangaza rasmi matokeo ya Senza ya watu na makazi na kutaja idadi kamili, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya, alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12, 313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012, ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002. 
 Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
 Kikundi cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
 Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
 Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na makazi.

KLABU ZA JOGGING JIJINI DAR ZAAGA MWAKA KWA BONANZA , MBUNGE WA KINONDONI ASHIRIKI AWAAMBIA HAKUNA SABABU YAKWENDA LOLIONDO MAZOEZI YANATOSHA.



Mbunge wa jimbo la Kinondoni Iddi Azzani, akiwapa mazoezi vijana wa Klabu Jogging 12 za maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam  wakati alipoalikwa kushiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Kabla ya bonanza hilo kulikuwa na mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilometa nana kutoka Kawe kupitia Lugalo hadi Mbezi Beach na kurejea kwa kupita barabara ya Bagamoyo ya zamani hadi.
Vijana wa Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni wakifanya mazoezi kwenye bonanza hilo.

Vijana wa jiji la Dar es Salaam kutoka kwenye Klabu za Jogging zipatazo 12 wakifanya mazoezi ya kukimbia mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam Kabla ya kuanza kwa Bonanza la kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013 lililoandaliwa na Klabu ya Jogging ya Kawe jijini humo.

Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni jijini Dar es Salaam ikivutwa na Timu ya Klabu ya Jogging ya Kawe na kuondolewa.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzani akishiriki mazoezi ya kukimbia ya umbali wa Kilometa nane yaliyofanywa na Klabu za Jogging jijini Dar es Salaam leo.
Pamoja na kuwepo kwa mvua vijana hao hawakuacha kufanya mazoezi.
Mvua si sababu ya kuacha mazoezi.

Iddi Azzani akiongoza timuyake ya Klabu ya Jogging ya Barafu ya Magomeni na kuibuka kidedea.
Vijana wakichangamsha damu asubuhi yaleo!

Katibu wa Kawe Jogging Klabu (Mdau) Razalo Ngimba (katikati) akiwa na Refaree maarufu nchini Othmani kazi (kulia) wakati wa mazoezi kabla ya bonanza kuanza.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...