Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, December 20, 2012

CHEKA KUPAMBANA NA MMALAWI DESEMBA 26Na Elizabeth John

KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)  imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi anayetokea katika jiji la Addis Ababa, Ethiopia.
Mpambano huo wa kimataifa unatarajia kufanyika Januari 26 mwakani, ambayo pia itakuwa ni siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit) katika jiji hilo la Abesinia.
Cheka na Chimwemwe watakutana mjini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG).

Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kwa kila raundi moja.
Mpambano wa Cheka na Chimwemwe umeandaliwa na Kampuni ya Screen Hills (T) Investment ya Dar es Salaam inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa Andrew George ‘Chagga Boy’.
Kwa mujibu wa Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi, umaarufu wa mabondia hao umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Afrika.
Mpambano huu umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...