Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 22, 2012

MAHAFALI YA NANE CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (SUZA) YAFANA LEO.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), akitoa hutuba yake baada ya kuwatunuku Shahada,katika sherehe za Mahafali ya nane ya chuo  zilizofanyika huko katika kampasi ya Tunguu leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), akitoa hutuba yake baada ya kuwatunuku Vyeti,Shahada
na Stashahada, wa fani mbali mbali wahitimi wa Chuo Kikuu cha SUZA, katika sherehe za Mahafali ya nane ya chuo zilizofanyika huko katika kampasi ya Tunguu leo
Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) wa fani mbali mbali wakiwa katika maandamano ya sherehe za mahafali ya nane ya  chuo hicho zilizofanyika leo katika kampasi ya Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Baadhi ya Viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioalikwa katika sherehe za Mahafali ya nane ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) zilizofanyika leo katika kamapasi ya Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...