Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 24, 2012

Dk. Didas Masaburi amejibu shutuma leo


BAADA ya Waziri wa  Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), kuwashukia viongozi wa jiji kuwa ndiyo chanzo cha kukithiri uchafu jijini, Meya wa jij

 Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, na Meya huyo wakati alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu kikao cha kufunga mwaka 2012.
 
Masaburi alisema kauli ya waziri huyo, inaonekana kujichanganya kwani kazi ya kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi siyo ya jiji bali wahusika wakuu ni Halmashauri.
 
Alisema kazi kubwa ya mamlaka ya jiji ni kusimamamia hali ya usafi usafi wa dampo liliko Pugu Kinyamwezi.
 
“Hizo lawama wanapaswa wazielekeze kwenye Halmashauri kutokana na wenyewe kushindwa kupeleka taka na siyo sisi jiji, kama wenyewe hawatuletei taka dampo na alaumiwe”alisema.
 
Dk Masaburi anastajabishwa, utaratibu unaotumiwa na baadhi ya mawaziri kwa kuzishambulia Halmashauri kuwa zinafuga uozo wa uchafuzi wa mazingira, ambapo hata huko kwenye  ofisi za wizara zao upo uchafu.
 
Alitoa wito kwa Serikalli Kuu kubadili utaratibu wake kwa kuzitengea fedha za kutosha Halmashauri hizo na kuzifikisha kwa wakati,  lengo likiwa ni kwenda sambamba na sheria ya mazingira ya mwaka 2004.
 
Alisema vyanzo ya mapato wakati mwingine vinaweza kuwa chanzo cha Halmashuri hizo kushindwa kusimamia sheria hiyo ya utunzaji wa mazingira.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...