Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, December 20, 2012

OMMY DIMPOZ ATOKA NA 'KOIKOI'Na Elizabeth John

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Koikoi’.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Ommy amesema anaamini wimbo huo utapokelewa vizuri na mashabiki wake kutokana na mashairi ya wimbo huo ni ya kuburudisha jamii inayomzunguka.
“Namshukuru mungu kazi zangu zote zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu, hivyo nimejipanga kutoa burudani iliyokwenda shule kwa kutumia kipaji changu ikiwa ni njia moja wapo ya kujivutia mashabiki wa kutosha,” amesema Ommy Dimpoz.
Amesema anawaomba mashabiki na wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea video ya kazi hiyo ambayo anatarajia kwenda kuitengeneza nje ya nchi.
Ommy Dimpoz kwasasa anatamba na nyimbo zake kama, Nai nai na Baadae ambazo zilimtambulisha na zinaendelea kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...