Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 24, 2012

AZAM FC YATWAA KOMBE LA UHAI 2012.


 Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu akimkabidhi nahodha wa timu ya Azam FC, Abdul Mgaya kombe la Ubingwa wa  michuano ya Uhai Cup 2012 baada ya timu hiyo kuifunga Coastal Union ya Tanga kwa penalti 3-1 katika mchezo wa fainali ya vijana chini ya miaka 20 uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Tenga.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah akimkabidhi zawadi ya mfungaji bora wa mashindano ya vijana chini ya miaka 20 ya Uhai Cup, Ramadhani Mkipalamoto wakati wa fainali ya michuano hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe lao
Golikipa wa Azam FC, Aishi Salum akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...