Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 31, 2012

KLABU ZA JOGGING JIJINI DAR ZAAGA MWAKA KWA BONANZA , MBUNGE WA KINONDONI ASHIRIKI AWAAMBIA HAKUNA SABABU YAKWENDA LOLIONDO MAZOEZI YANATOSHA.Mbunge wa jimbo la Kinondoni Iddi Azzani, akiwapa mazoezi vijana wa Klabu Jogging 12 za maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam  wakati alipoalikwa kushiriki Bonanza la kumaliza mwaka lililoandaliwa na Kawe Jogging Klabu na kufanyika leo jijini Dar es Salaam. Kabla ya bonanza hilo kulikuwa na mazoezi ya kukimbia umbali wa Kilometa nana kutoka Kawe kupitia Lugalo hadi Mbezi Beach na kurejea kwa kupita barabara ya Bagamoyo ya zamani hadi.
Vijana wa Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni wakifanya mazoezi kwenye bonanza hilo.

Vijana wa jiji la Dar es Salaam kutoka kwenye Klabu za Jogging zipatazo 12 wakifanya mazoezi ya kukimbia mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam Kabla ya kuanza kwa Bonanza la kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013 lililoandaliwa na Klabu ya Jogging ya Kawe jijini humo.

Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni jijini Dar es Salaam ikivutwa na Timu ya Klabu ya Jogging ya Kawe na kuondolewa.
Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzani akishiriki mazoezi ya kukimbia ya umbali wa Kilometa nane yaliyofanywa na Klabu za Jogging jijini Dar es Salaam leo.
Pamoja na kuwepo kwa mvua vijana hao hawakuacha kufanya mazoezi.
Mvua si sababu ya kuacha mazoezi.

Iddi Azzani akiongoza timuyake ya Klabu ya Jogging ya Barafu ya Magomeni na kuibuka kidedea.
Vijana wakichangamsha damu asubuhi yaleo!

Katibu wa Kawe Jogging Klabu (Mdau) Razalo Ngimba (katikati) akiwa na Refaree maarufu nchini Othmani kazi (kulia) wakati wa mazoezi kabla ya bonanza kuanza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...