Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 31, 2012

IJUMAA YA MWISHO KWA MWAKA 2012 SKYLIGHT BAND YAVUMBUA KIPAJI KIPYA NI MSHINDI WA PILI WA EBSS 2012 SALMA YUSUF


Sam Machozi a..k.a Sam Mapenzi akiongozaji waimbaji wenzake Aneth Kushaba (kushoto) sambamba na Sony Masamba wakitoa burudani ya aina yake Ijumaa ya mwisho kwa mwaka 2012 katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. 
Sura mpya ya SKYLIGHT Band ikifanya yake Jukwaani katika show ya mwisho ya Band hiyo kwa Mwaka 2012 iliyofanyika Ijumaa ya tarehe 28 mwezi huu katika kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar es Salaam. Si mwingine ni Binti mdogo mwenye kipaji cha aina yake mshindi wa pili katika shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 Salma Yusuf sambamba na Meneja wa Band hiyo Aneth Kushaba AK 47 wakiwapa raha mashabiki wa bendi hiyo.
Carolina mama njoo tucheze pamoja..... Moja ngoma inayobamba mujini ya SKYLIGHT BAND katia vituo mbalimbali vya radio hapa nchini. Mungu akipenda Usikose Ijumaa hii ya kwanza kwa Mwaka 2013.
Palikuwa hapatoshi..... kwa raha zao.
"Gere Mama Gere..... Wanionea Gere....." Binti mwenye kipaji sauti ya kasuku Salma Yusuf akiwazungusha mashabiki wa SKYLIGHT BAND kwa mduara akipigwa tafu na Joniko Flower pamoja na Sony Masamba katika ukumbi wa Thai Village jijini Dar.
Pichani Juu na Chini Wake kwa Waume wakizungusha mduara huku wengine wakimwaga radhi hapo kati..Hapo chacha.
Chezea Salma Yusuf wewe ulizoe kumuona kwenye TV wakati wa EBSS 2012 njoo umuone Live Ijumaa akitambulishwa rasmi kwa mashabiki wa SKYLIGHT BAND.
Wadau wakishow love katika ukumbi Thai Village Masaki jijini Dar.
Vijana Watanashati wakipata Ukodak...Single Ladies mpooooo??? Kazi kwenu.
SKYLIGHT BAND ilipata ugeni kutoka The B Band ya Banana Zorro. Pichani ni Aneth Kushaba AK 47 akishow love na baadhi ya wasanii wa The B BAND.
Mdau King Kif akishow Love na Aunty Ezekiel a.k.a Mrs. Demonte pamoja na rafiki yake katika usiku wa SKYLIGHT BAND.
Mdau Eric Ndalu katika pozi.
Kati ya Vijana hawa wawili walikuwa wakisheherekea siku yao ya kuzaliwa ndani ya Kiota cha Thai Village na SKYLIGHT BAND.
Wadau wakipata Ukodak mbele ya Camera yetu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...