Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 26, 2012

NDONGA ZA MWAKA DAR LIVE: WATANZANIA WATOA KICHAPO KWA WAPINZANI WAO
Mada Maugo (kushoto) akimshushia kichapo bondia Yiga Juma (Uganda) wakati wa mpambano wao.
Bondia Mbwana Matumla (kulia) akitupiana makonde na bondia David Charanga kutoka Kenya.
Bondia David Charanga kutoka Kenya (kulia) akienda chini baada ya kupokea konde kutoka kwa Mbwana Matumla.
David Charanga kutoka Kenya (kulia) akimkabili bondia Mbwana Matumla wakati wa mpambano wao jana.
--
Mabondia wa Tanzania jana waling'ara katika mapambano yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem. Bondia maarufu nchini, Mada Maugo alimchapa Yiga Juma kutoka Uganda raundi ya kwanza kwa ‘Knock Out’. Katika hali iliyoonesha kuwa siku ya vichapo kwa wageni, pambano lingine ambalo bondia Mbwana Matumla alipambana na bondia kutoka Kenya, David Charanga lililokuwa la raundi nane, Matumla aliibuka kidedea katika raundi zote nane na kumfanya aibuke na ushindi wa kishindo.
(PICHA NA ISSA MNALLY NA RICHARD
Bondia Mada Maugo (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumtwanga bondia Yiga Juma (Uganda) kwa KO raundi ya kwanza.
Bondia Mbwana Matumla (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumpa kichapo bondia David Charanga (Kenya).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...