Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, December 27, 2012

CHEKA AWAPA RAHA MASHABIKI WA NGUMI JIJI LA ARUSHAMeya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo na rais wa TPBC Onesmo Ngowi wakimvisha mkanda Francis Cheka

Francis Cheka akiongea na waandishi wa Habari baada ya pambano kumalizika


Frincis Cheka akikwepa konde la Chimwemwe

Jaji Boniface Wambura akitafakari kitu kabla mpambano kuanza
Bondia Francis Cheka leo ametwaa ubingwa wa IBF Afrika baada ya kumpiga kwa pointi bondia toka Malawi Chiotka Chimwemwe kwenye pambano la raundi 12 lililofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Majaji wa pambano hilo ambao walikuwa watatu walitoa maksi kama ifuatavyo: David Chikwanje alimpa Cheka pointi 112/114 za Chimwemwe, Boniface Wambura alimpa Cheka pointi  118/114 za Chimwemwe na James Ligongo alimpa Cheka pointi  120/115 za Chimwemwe


Cheka ambaye alipigwa konde la haja likasababishwa kuchanika katikati ya paji la uso raundi ya pili aliweza kuhimili kumaliza raundi zote huku akitibiwa kila saa.


Baada ya Mpambano kumalizika Cheka allisema anashukuru ameshinda ila mpambano ulikuwa mgumu sana kwake na alikiri hajakutana na bondia mkali kama Chimwemwe kwa karibuni.

 "Nashukuru nimeshinda ila nimeshinda kwa bahati kwani bondia niliyekutana naye ni bondia mzuri kwani angeweza kushinda ila alikosa mbinu chache tu", alisema Cheka.

Naye bondia Chiotka Chimwemwe alikubali matokeo na kusema ni mara yake ya kwanza kupigana nje ya nchi yake  hivyo amechukulia kama changamoto kwake.


Cheka ameweza kutwaa Ubingwa wa IBF Afrika baada ya kunyang'anywa kwa kushindwa kuutetea kwa muda na akaenda kucheza na Karama Nyilawila ubingwa wa UBO ambao pia alimpiga Nyilawila.


Naye Meya wa jijini la Arusha  Gaudence Lyimo alimpongeza promota wa pambano hilo Andrew George na Rais wa TPBC Onesmo Ngowi kwa kuleta pambano hilo la kimataifa Arusha na kusema atashirikiana nao kuwahakikisha anainua mchezo wa ngumi Arusha.


"Nawapongeza walioleta pambano hili Arusha na wnawaahidi tutakuwa tukishirikiana bega kwa bega kuahakikisha tunainua mchezo wa ngumi Arusha", alisema Meya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...