Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 29, 2012

SIMBA SC YATANDIKWA 3-0 NA TUSKER YA KENYA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM


 
Mshambuliaji wa Simba Uhuru Seleman akiwani mpira dhidi ya kiungo wa Tusker ya Kenya Joseph Mbugi wakati wa mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na Simba kukubali kutandikwa bao 3-0.


SIMBA SC imefungwa mabao 3-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Katika mchezo huo, uliochezeshwa vema na refa Hashim Abdallah, hadi mapumziko, tayari Tusker walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Jesse Were dakika ya 37 na 45.
Mabao yote yalitokana na udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba, ambayo hii leo iliongozwa na beki kutoka Mali, Komabil Keita kiasi cha kufikia mfungaji anafunga akiwa amebaki anatazamana na kipa.
Simba ilikuwa ikishambulia kutokea pembeni, lakini mipira mingi mirefu iliyokuwa inamiminwa langoni mwa Tusker ilikuwa inaokolewa na mabeki warefu wa klabu hiyo bingwa ya Kenya, wakiongozwa na beki wa zamani wa Yanga, Joseph Shikokoti.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi kwa nguvu tena na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 54, mfungaji Frederick Onyango.
Simba pamoja na kufanya mabadiliko, ikiwatoa Haruna Shamte, Haruna Athumani, Paul Ngalema, Mussa Mudde, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhani Chombo na Kiggi Makassy na kuwaingiza Miraj Adam, Hassan Isihaka, Emily Ngeta, Jonas Mkude, Salim Kinje, Haruna Moshi, Ramadhani Singano, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Edward Christopher, haikuweza kupata hata bao la kufutia machozi.
Nassor Masoud aliingia kuchukua nafasi ya Shamte, lakini naye akaumia na kutoka nafasi yake ikichukuliwa na kinda wa Simba, B, Masele Kaheza.
Simba SC; William Mweta, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Hassan Khatibu, Komabil Keita, Mussa Mude, Haroun Athumani, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhan Chombo na Kiggi Makassy.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Frederick Onyango, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...