Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 19, 2012

Smile You are with Tigo Press Release

Dar es Salaam,Tanzania 18 Desemba, 2012. Tigo ina madhumuni ya kuweka tabasamu kwenye kila uso wa mteja wake wa Tanzania, kupitia bidhaa na huduma zake bunifu na kwa kuendelea kuwapa wateja wake kipaumbele kwenye mahitaji yao maalum, nchi nzima.
Kwa maana hii Tigo Tanzania, mtandao wa bei nafuu , unaopatikana kote nchini kwa urahisi , unabadilisha slogan yake kutoka “Express Yourself” kwenda ‘’Smile You’ve got Tigo” , yaani tabasamu upo na Tigo. 
Slogan hii mpya inaonesha vile wateja wetu wanavyoridhika na aina mbali mbali ya bidhaa zetu ambazo zipo sokoni, zinazoboresha maisha yao na kuwasaidia kwenye shughuli zao za kila siku. Huduma kama Tigo Pesa zinazorahisisha utumaji na upokeaji wa fedha nchi nzima.Tigo Telco Solutions  maalum kwa wafanyabiashara, na hivi karibuni Tigo imetoa vifaa vya nishati vya jua kwa kuchaji simu . Mradi huu unatoa ufumbuzi kwa maeneo yasiyo na umeme, unasaidia ujasiriamali na wakati huohuo unaokoa mazingira kwa kutumia nishati rafiki isiyoathiri mazingira.
Programu kubwa ya Tigo ya kurejesha kwa jamii ‘Reach for Change’ inasaidia wajasiriamali wa miradi ya kijamii na itawagusa watoto na vijana wengi wa kiTanzania.
‘’Hizi programu,bidhaa na huduma, na nimegusia chache tuu, bila shaka zimeweka tabasamu kwenye nyuso za wateja wetu. Pia kupewa nafasi ya juu kimataifa, kwenye huduma kwa wateja kupitia mtandao wetu, inaoyesha kwamba juhudi zetu zinaonekana na zinakubalika.” Alisema Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez.
Tigo inataka kuwapa wateja  njia ya kujieleza na zaidi .
 ‘’Tigo Tanzania inalenga kuwapa wateja wake bidhaa, huduma bora , na mtandao wa uhakika. mbali mbali, mtandao na huduma kwa wateja bora .Kibiashara Tupo kwenye familia ambayo inatoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 43 dunia nzima , na tunataka wateja wetu wawe na raha na kutabasamu kwasababu wana mtandao wa Tigo” alisema Bwana Gutierrez.
Kuhusu Tigo
 
Tigo ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 tanzania Bara na Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshwaji wa huduma zake za simu nchini Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano  mpaka katika kutoa huduma za intanet zenye kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu kupitia  Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

1 comment:

  1. I'm curious to find out what blog system you have been using? I'm experienсing somе small security іѕsuеѕ ωіth mу lateѕt wеbsite and
    I ωould lіkе to fіnԁ sοmething mоre secuгe.

    Dο уou haѵe anу recommenԁations?


    Αlsο vіsіt my web blog natural breast augmentation

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...