Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 31, 2012

BREAKING NEEEWZ!! RAIS WA MAKAPERA TANZANIA ISSA KWISSA MWAIFUGE AJIUZULU UKAPERA AWAGEUKA WENZAKE GHAFLA AOA RASMI LEO


 Rais wa Makapera Tanzania, Issa Kwisa Mwaifuge, leo ameamua kuwageuka wafuasi wake rasmi na kuvunja katiba ya kundi lake na kuamua kuuaga ukapera rasmi na kumuoa Binti mrembo aliyewahi kushiriki shindano kubwa la Miss Tanzania, 2004, Verdiana Kamugisha, ambao kwa pamoja wameamua kumeremeta siku ya leo na kufunga ndoa yao katika Kanisa la Lutheran lililopo mitaa ya Sinza jijini Dar es Salaam. Na hapa ni wakati wakiwa katika sherehe ya ndoa yao inayoendelea muda huu katika Ukumbi wa Msasani Makuni. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
 Bwana Harusi, Issa Kwisa (kushoto) akisebeneka na Suleiman Semunyu, aliyekuwa akipokea zawadi ya keki kwa niaba ya ITV.
 Maharusi, wakipozi kwa picha na wafanyakazi wa Star Tv, baada ya kuwakabidhi zawadi ya keki.
 Hapa ilikuwa ni muda wa Kwaito..........
 Sehemu ya wageni waalikwa.....
 Wadau kutoka (kulia) ni James Range, Joseph Mpangala na Martine Mauya, wakipozi kwa picha mbele ya kamera ya Sufiaimafoto.
 Baadhi ya wafanyakazi wa ITV ambao ni wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi, wakipozi kwa picha, baada ya kukabidhiwa zawadi ya keki na Bwana harusi.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Chanel Ten, wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi ya Keki.
 Sehemu ya wageni waalikwa,..
Salum Mkambala, akisebeneka kwa staili yake wakati akielekea kupokea zawadi ya keki kwa niaba ya wafanyakazi wenzake wa Chanel Ten.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...