Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 26, 2013

RAMADHAN KIDO AOMBA KURUDIANA NA MCHUMIATUMBO 'ARIVENJI'


BAADA ya kuchapwa katika mchezo wao wa kwanza uliokuwa na kila aina ya majigambo kwa mabondia, Ramadhan Kido na Mchumiatumbo, hatimaye sasa bondia mbavu nene Ramadhan Kido, anasema kuwa anamhitaji tena mbavunene mwenzake Alphonce mchumiatumbo, ili aweze kumuonyehs akuwa alimuotea na kumchapa kwa bahati mbaya katika mchezo wao ulipita.

Mabondia hao walichapana katika pambano lao la kwanza lililofanyika uwanja taifa na kumalizika kwa Bondia Kido, aliyekuwa amedhaminiwa na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, kuchapwa kwa KO,ambapo sasa amepania kulipa kisasi.

''Mchumiatumbo amenifanya nameshindwa kulala kwa muda mrefu sana tangu aliponipiga katika pambano lililopita, jambo ambalo limenifanya kujifua kufa na kupona kujiweka fiti ili niombe marudiano niweze kurivenji.

Siku zote nimekuwa nikimfikiria yeye kanipigajepigaje jibu sipati,nimeamua kurudi tena ulingoni kwa kujipima na Mussa Mbabe, katika pambano letu litakalofanyika siku ya jumapili Aprili 7, mwaka huu katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala.

Najua Musa ni bondia mzuri lakini siwezi kupoteza mara mbili mfululizo huu ni mwiko wangu nitahakikisha nafia ulingoni na ntajituma  kwa nguvu zangu zote na kuhakikisha namchapa kwa KO mbaya, bila huruma hata nikiua sawa tu nina uchungu sana na ngumi na nataka nimuoneshe Mchumiatumbo kuwa nakuja kivingine,na nikipigwa katika pambano la mwananyamala ni bora niache ngumi kabla ya kurudiana na Mchumiatumbo''. alisema Kido

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...