Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 29, 2013

BONDIA IDDY MKWERA AMCHIMBIA MKWALA LUCAS NDULA WA MUHEZA
IDDY MKWERA
BONDIA Iddy Mkwera wa Dar es salaam anatarajia kuzipiga na Lucas Ndula wa Muheza wakati wa kusherekea sikukuu za pasaka jumapili ya march 31 katika viwanja vya wazi vya Jitegemee vilivyopo wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga
Bondia huyo  aliyefika Muheza kwa mbwembwe na kusema atamtwanga
Ndula
K,O ya raundi ya pili ili arudi na ushindi Dar es salaam kwa ushindi mnono unajua mimi nafundishwa na kocha wa kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D'  anaejua mbinu zote za masumbwi Duniani na nimefanyia mazoezi miezi miwili hivyo sitarajii kuremba katika mpambano huo kwani kwa sasa nimeamua kucheza mchezo huu na ninawambia mabondia wote walio katika uzito wa kg, 60 kuwa tayali kupambana na mimi

Mchezo huo utakaochezwa katika viwanja vya jitegemee Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga utakuwa na bule hivyo watu mbalimbali wameobwa kujitokeza kuja kuangalia vipaji vya mchezo huo wenye kupendwa na vijana wengi nchini

Nae mmoja wa wadau wa nchezo wa ngumi Muheza Allan Augastino ambaye aliyetoa galama mbalimbali amesema vijana wengi wanapenda ngumi hivyo nimeamua kuwaletea hapa hapa bila kujali chochote na kugalamia kila kitu ikiwemo mabondia kutoka Dar pamoja na ulingo  maalumu kwa ajili ya kuchezea

Mbali na mbambano uho kutakua na mapambano mengine mbali mbali ambapo Omari Kibwana wa dar atapambana na
Bakari Sendekwa

  Nae kocha wa mchezo huo Muheza, Chalres Muhilu ' Spins' alisema mpambano huo wa wazi umeandaliwa kwa ajili ya kutoa burudani wilayani hapo na kuhamasisha mchezo wa masumbwi

mabondia kutoka Dar wakipambana na Muheza pamoja na kutoa rai kujitokeza kwa wafadhili kudhamini mchezo huo unaopendwa na vijana wengi wilayani humo ndio mana tumeamua kuweka katika viwanja vya wazi ili watu wote wajionee wenyewe mchezo wa ngumi unavyo endeshwa katika mazingira magumu

Nae Kocha wa kimataifa wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' aliyepewa jukumu la kwenda na vijana kutoka Dar ili wakalete changamoto na kuleta amasa ya mchezo huo amesema atakwenda na Omary Kibwana  atakayemenyana na Bakari Sendekwa katika uzito wa kilo 52 na Iddy Mkwera atakaepambana na Lucas Ndula mpambano wa raundi 6

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...