Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 27, 2013

DOUBLETREE BY HILTON YAKABIDHI TAA ZA KUTUMIA MIONZI YA JUA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MIKOCHENI A


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mikocheni A jijini Dar es Salaam, Salehe Makwiro (kulia) akipokea sehemu ya msaada wa taa 200 za kutumia mionzi ya jua kwa ajili ya wananfunzi wa darasa la saba ambao watazitumia kwa ajili ya kujisomea. Kulia ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Doubletree by Hilton, Florenso Kirambata na Meneja Mkuu wa Doubletree by Hilton, Sven Lippinghof.
Meneja Mkuu wa Doubletree by Hilton, Sven Lippinghof akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A jijini Dar es Salaam jinsi ya kutumia taa zinazotumia mionzi ya juu mara baada ya kukabidhi taa 200 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo.
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Doubletree by Hilton, Florenso Kirambata akiwafundisha jinsi ya kutumia taa zinazotumia mionzi ya jua wanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A jijini Dar es Salaam leo, wakati uongozi wa hoteli yhiyo ulipokabidhi msaada wa taa 200 kwa wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo kwa ajili ya kuwasaidia wakati wa kusoma. (Picha na Habari Mseto Blog)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...