Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 21, 2013

SHOO YA USIKU WA MAHAKAMA YA MAPENZI KULINDIMA MAISHA CLUB JUMAPILI
Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’ anatarajia kufanya shoo inayokwenda kwa jina la ‘Usiku wa Mahakama ya mapenzi’ Jumapili katika ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam.
Mahakama ya Mapenzi ni kati ya nyimbo za msanii huyo ambayo inafanya vizuri katika soko hilo kutokana na mashairi yaliyobeba ngoma hiyo.
Akizungumza na jijini Dar es Salaam jana, linex alisema katika shoo hiyo atasindikizwa na wakali wa muziki huo, H.Baba, Banana Zorro, Kala Jeremiah na wengineo.
Akizungumzia kuhusu uandaaji wa video ya kazi hiyo, Linex alisema kuna watu ambao ni raia wa Europe ambao anataka kushirikiana nao katika video hiyo na sasa yupo katika hatua za mwisho za kukamilisha mazungumzo.
“Unajua msanii unatakiwa kuwa mbunifu, hivyo nilipenda video ya kazi hii nifanye na watu hao ambapo tukielewana itakua hivyo, na ikishindikana nifanya na Adamu Juma,” alisema Linex.
Mbali na hayo Linex alisema kwasasa ameamua kufanya kazi na wasanii wakike ili kuwapa sapoti katika kazi zao na kukuza muziki huo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...