Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 19, 2013

MSANII SNURA MUSHI ATANGAZA KUSAKA MUME AMBAYE HATAMBANA......


MSANII wa filamu na muziki mwenye mvuto wa aina yake Snura Mushi ‘Snura’, ameamua kutoa la moyoni kwa madai kuwa sasa anatafuta mwanaume wa kuweza kufunga naye pingu za maisha lakini kwanza kabisa akubali kumpa muda mrefu wa kutafuta pesa ili asiwe tegemezi baada ya kuingia ndani ya ndoa hiyo.


Kauli ya msanii huyu imekuja mara baada ya mwandishi wetu kumswalika maswali kadhaa kuhusiana na mikakati ya maisha yake ya muziki na mahusiano .....


Akiongea kwa mbwembwe, Snura alidai si kwamba hataki kuolewa bali hataki kuishi ndani ya ndoa na kuwa tegemezi kwa mwanaume.


“Sitaki kuishi na mwanaume kabla hajakubali kunipa muda wa mimi kutafuta pesa...


Najua anaweza kuwa na uwezo wa kila kitu lakini hivyo vyote vitakuwa vya kwake na mimi natakiwa kuwa na mali zangu, lakini bila hivyo nitazeekea kwangu,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...