Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, July 25, 2013

MSONDO NGOMA MUSIC YAINGIA STUDIO NA KUTANGAZA RATIBA YA IDDI

SUPER D
BENDI Kongwe ya Mziki wa dansi nchini Msondo Ngoma imeingia Studio kurekodi nyimbo zake mpya zitakazokuwa katika Albam moja akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Bendi Hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa bendi yake kwa sasa imeingia studio kukamilisha kurekodi nyimbo zao mpya
Alizitaja nyimbo hizo kuwa li Suluhu uliotungwa na Shabani Dede,Lipi Jema na Baba Kibebe wa Eddo Sanga,Nadhili ya mapenzi wa Juma Katundu,Kwa momba akuna Uridhi ,Machimbo nyimbo zote hizo zikikamilika zitawekwa kwenye albam moja kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wao wawapo majumbani

Super D aliongeza kuwa bendi hiyo kwa sasa imesimamisha maonesho yake lakini watakapoanza sikukuu ya Idi mosi watatoa burudani katika ukumbi wa DDC Kariakoo idi pili watakua TTC Chang'ombe na idi tatu watavuka bahari kuelekea visiwa vya karafuu na kufanya onesho lao Zanzibar


Bondi hiyo kwa sasa inatamba na nyimbo zake mbalimbali wameweka nia ya kukonga mashabiki wa bendi hiyo kwa kupiga nyimbo mpya na zazamani ili kila mtu apate burudani unajua bendi yetu kongwe lazima tutoe burudani za aina tofauta aliongeza Super D

Bendi hiyo iliyopata umarufu mkubwa miaka ya nyuma imewahakikishia wapenzi wake kurudi katika ubora ule ule kama ilivyokuwa awari

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...