Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, July 12, 2013

AMINI KAIBUKA NA 'WHY MIMI'


Na Elizabeth John
Pia alisema anatanguliza audio kwa lengo la kuwaweka sawa mashabiki wake, ikiwa ni pamoja na kuwatayarisha kwa ajili ya kazi zake nyingine ambazo zinakuja hivi karibuni.


MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, anatarajiwa kuachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Why Mimi’.
Amini, amesema katika kazi hiyo ameshirikiana vyema na msanii Barnaba Elias iBarnaba Boy’ anaamini kazi hiyo itapokelewa vyema na kushika chati katika tasnia ya muziki huo kutokana na uwepo wa mwanamuziki huyo anae bamba katika tasnia hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Amini alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho amekitengeneza katika Studio ya Surround Records chini ya mtayarishaji wake maarufu, Emma The Boy.
“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwa ajili ya kukipokea kibao hiki, ambacho naamini kitaelimisha na kuburudisha jamii inayotuzunguka,” alisema Amini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...