Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 28, 2013

BERRY BLACK AIBUKA NA 'ISHARA ZANGU'
Na Elizabeth John
BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Berry Black ameibuka upya na anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ishara zangu’ hivi karibuni.
Berry Black alishawahi kutamba na ngoma yake ya ‘Naomba nisamee’ ambayo ilifanya vizuri miaka ya nyuma na kulitangaza vema jina lake katika tasnia ya muziki huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Berry Black alisema katika ngoma hiyo kamshirikisha nyota wa muziki huo, Alikiba.
“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea ngoma hiyo ambayo naamini itafanya vizuri kutokana na uwepo wa mkali huyo pamoja na kusimama kwa mashairi ya kazi hiyo,” alisema.

Berry Black alisema anaomba mashabiki wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hiyo ambayo anatarajia kuitoa pamoja na video yake akiwa na lengo la kuwapa burudani iliyokamilika wapenzi wake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...