Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 28, 2013

'KIBUDU' CHA MSECHU CHAFANYA KWELI

Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Peter Msechu, ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Kibudu’ ambacho kimeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Mbali na kutamba na kibao hicho, mkali huyo alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Relax’, ‘Kumbe’ ambavyo vilifanya vizuri zaidi mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vilimtambulisha katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msechu alisema kazi hiyo imekamilika na tayari imeanza kufanya vizuri katik avituo mbalimbali vya redio.

Alisema kibao hicho kakitengeneza katika studio ya Ufundi Production chini ya mtayarishaji wake mahiri, Fundi Samuel.

“Naomba mashabiki wangu wakipokee vizuri kibao hicho ambacho natarajia kukifanyia video yake Nairobi, Kenya,” alisema.


Msechu aliwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya video hiyo ambayo anatarajia kuitoa mwinzoni mwa mwezi ujao ikiwa ni pamoja na nyimbo nyingine nyingi zinazofuata.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...