Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 28, 2013

DOGO JANJA AJIPANGA 'KUSEREBUKA'
Na Elizabeth John

KINDA anayetamba katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ anatarajiwa kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Serebuka’ hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dogo Janja alisema ngoma hiyo ameshaikamilisha na anatarajia kuanza kuisambaza katika vituo mbalimbali wiki ijayo.

Alisema yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho ambacho anaamini kitakonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo ndani na nje ya nchi kutokana na ubora wa mashairi yaliyopo ndani yake.

“Namshukuru Mungu kazi zangu huwa zinapokewa vizuri na mashabiki wangu, kitu ambacho kinanipa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika ‘game’, hivyo nawaomba mashabiki wa kazi zangu waendelee kusubiri vitu vizuri kutoka kwangu,” alisema Dogo Janja.


Mbali na kibao hicho, Dogo Janja kwasasa anatamba na kibao chake cha ‘Maisha ya Skonga’ ambacho ameshirikiana vema na mwaamuziki kutoka kundi la Watanashati, PNC na kwamba ameamua kushirikiana naye kutokana na uwezo wake katika tasnia ya muziki, ikiwa ni pamoja na historia yake nzuri ya kuutangaza muziki wa Bongo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...