Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 28, 2013

AT 'ANAPENDA'

Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Kitumbua’, mkali wa muziki wa mduara nchini, Ally Ramadhan 'AT' anatarajia kuachia kazi mpya inayokwenda kwa jina la ‘Anapenda’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, nyota huyo alisema kazi hiyo anatarajia kuisambaza katika vituo mbalimbali vya radio baada ya kukamilika.

“Nashukuru Mungu kupata nafasi nyingine tena ya kurudi katika kazi yangu baada ya kimya kisichojulikana," alisema.

Msanii huyo ambaye anajulikana kama mfalume wa muziki huo kwa sasa alifanya vizuri na vibao mbalimbali kikiwemo Kifuu Tundu, Bao la Kate na nyinginezo ambazo zilimpa umaarufu mkubwa katika tasnia ya muziki huo.

Pia mkali huyo yuko katika hatua za mwisho kukamilisha video ya kazi yake inayoitwa ‘Kitumbua’, ambayo muda wote itaanza kuonekana kupitia kwenye runinga runinga na akiamini utapata nafasi kubwa ya kuwakonga mashabiki wa tasnia hiyo.


Hivyo, aliwaomba mashabiki kumuunga mkono katika kazi zake zijazo ili kuhakikisha anafikia malengo aliyojiwekea katika tasnia hiyo ya muziki wa kizazi kipya nchini hususan wa ‘Mduara’ ambao anaendelea kufanya vizuri na kutishia waliopo kwenye burudani hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...