Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, July 20, 2013

MICHUANO YA KOMBE LA MUUNGANO MUFINDI KILELE LEO ,MADIWANI MUFINDI WAKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA BAADA YA MADIWANI MANISPAA YA IRINGA KUINGIA MITINI Mratibu  wa  kombe la  Muungano Mufindi Daus Yassin , Kulia akikabidhi  kombe la  ubingwa kwa  wachezaji wa  timu ya Madiwani  Mufindi baada ya  kuibuka na ushindi wa bure  kufuatia  timu ya madiwani Manispaa ya Iringa  kuingia mitini  bila kufika  uwanjani katika mchezo wa  kirafiki  wa  utangulizi uliopaswa  kupigwa  uwanja  wa shule ya Msingi  Wambi mchana  wa leo 
 Mratibu  wa  kombe la muungano Mufindi akishuhudia  furaha za madiwani Mufindi  baada ya  kukabidhiwa  kombe la ubingwa
 Madiwani  Mufindi  wakishangilia  ubingwa  wao  wa  bure  baada ya madiwani wa manispaa ya  Iringa  kushindwa  kufika uwanjani  leo

Mbunge  wa jimbo la Mufindi kusini Medrad Kigolla kushoto akiwa na timu yake ya madiwani Mufindi , Mchezo  unaofuata  jioni hii ni kati ya  Mbeya  City na Mbaspo  zote  kutoka  Mbeya
 Timu ya madiwani  Mufindi katika  picha ya pamoja na  timu ya  Veterani Mufindi  ambao  wamelazimika kucheza mchezo  wa kirafiki wa  kuvuta mashabiki  uwanjani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...