Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 17, 2013

MAKAMU WA RAIS KUFUNGA KOZI CHUO CHA ULINZI WA TAIFA


Mkamu wa Rais
Chuo cha Ulinzi wa Taifa (National Defence College), kinatarajia kufunga kozi kwa wahitimu kundi la kwanza wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa kwa  mwaka 12/13.

Sherehe hiyo itafanyika  tarehe 20 Julai 2013 kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Hii ni mara ya kwanza kwa chuo hicho kutoa wahitimu toka kilipoanza kuendesha kozi zake mwaka 2012.

Tafrija hiyo itafanyika Kunduchi Dar es salaam mahali kilipo chuo hicho, ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Gharib Bilal.

Aidha, watakuwepo viongozi  wa Kitaifa, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wadau wengine .

Vyombo vya habari vinaalikwa kushiriki katika tukio hilo ambalo ni muhimu kwa Taifa.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764742161
Email: ulinzimagazine@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...