Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 15, 2010

MANNY PACQUIAO AENDELEZA UBABEBONDIA Manny Pacquiao ameweza kutetea ubingwa wake baada ya kumtwanga Antonio Margarito kwa pointi katika pambano lilichezwa Jumamosi usiku.

Pambano hilo lilihudhuriwa na mashabiki 41,734 katika uwanja wa Cowboys, Pacquiao alionyesha uwezo kwa yeye ni bondia mzuri duniani kwa kuweza kutawala sehemu kubwa ya mchezo lakini mpinzani wake Margarito alivumilia na kumaliza raunsi zote.

Pacquiao aliongoza randi moja baada ya nyingine, alimpasua Margarito kidevuni na kufanya jicho la kulia kuvimba kutokana na kichapo.

Pacquiao ambaye ni mbunge nchini Ufilipino alionyesha uwezo wake wa kupiga ngumi kwa kasi.

Margarito alijitajia kujaribu kumtuliza Pacquiao ulingoni lakini kila alipokuwa akimkaribia mpinzani wake alikuwa akirusha ngumi nne hadi tano kichwani kwake na kuvuruga mipango yake.

Mbunge huyo alimfuata mara kadhaa refa Laurence Cole raundi ya 11 kumtaka kumaliza pambano baada ya kuona mpinzani wake akiwa amezidiwa lakini mechi iliendelea.

“Siwezi kuamini kumpiga bondia mkubwa na mwenye nguvu,” Pacquiao alisema. “Ilikuwa ngumu. Nilifanya kila ninaloweza kushinda mechi hii.”

Margaritto alisema kuwa hakutaka kujiuzuru katika mechi yao, ila kupambana hadi mwisho.

Pacquiao alipewa alama nyingi kutoka kwa majazi wote, 120-108, 119-109 na 118-110.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...