Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 15, 2010

GRAND MALT YATANGAZA UDHAMINI WA TAMASHA KUBWA LA VYUO VIKUU VYA DAR ES SALAAMKampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malt leo imetangaza rasmi kudhamini tamasha kubwa la burudani litakalovishirikisha vyuo zaidi ya 20 vya elimu ya juu vilivyopo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Meneja wa Grand malt Bi Cosolata Adam alisema tamasha hilo ni moja kati ya matamasha makubwa ambayo yanalenga kuwakuwakutanisha wasomi katika nyanja ya burudani lakini pia kuwakaribisha wana vyuo wapya wanajiunga kuanza mwaka wa kwanza wa masomo wa 2010/2011.

Alisema tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya TCC Club Chang”ombe siku ya jumamosi ya tarehe 20 November 2010 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni hivyo kuwaomba wanavyuo wote kushiriki kwa wingi katika tamasha hilo ambalo HALITAKUWA NA KIINGILIO CHOCHOTE.

Alisema Grand Malt imeamua kudhamini tamasha hilo kutokana na kuthamini na kutambua mchango wa wanavyuo kiujumla na umuhimu wao katika ujenzi wa Taifai hivyo kuana umuhimu wa kuwakutanisha na kwa pamoja kushiriki kwenye michezo mbalimbali ikiongozwa na buruni tofautitofauti zitakazokuwa katika tamasha hilo.


Bi Consolata aliwataka wanavyuo kutumia vyema tamasha hilo kwa kushiriki katika michezo mbambali na pia kuweza kupata wasaa wa kubadilishana mawazo miongoni mwa wanavyuo wa chuo kimoja na kingine.


Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo bwana Innocent Melleck alisema maandalizi kwaajili ya tamasha hilo yamekamilika kwa kiwango kikubwa na kilichobakia ni siku pekee ya kufanyika kwa tamasha hilo.


Alisema tamasha hilo ambalo linashirikisha wanavyuo walio katika vyuo vya elimu ya juu jijini Dar es salaaa linajulikana kwa jina la INTELLECTUALS GRAND BONANZA 2010 litaongozwa na wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya wanaotamba katika ulingo wa burudani nchini hivi sasa ikiwa ni pamoja na kundi zima la wanaume Familly (TMK) chini ya Mheshimiwa Temba na Chege mtoto wa mama Said na Crew nzima ya kundi hilo, lakini pia mwanamuziki Chid Benz atafanya vitu vyake katika kuhakikisha wanavyuo wanapata burudani ya kipekee kwa wakati wote huku mtangazaji mahiri wa kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha Redio cha Africa Mashariki (East Africa Radio) bwana Dullah Hamis Ambua atakuwa akisherehesha kwa wakati wote.


Bwana Melleck alisema pamoja na wanamuziki hao lakini pia wanavyuo wenye vipaji vya kuimba watapatiwa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa kupanda jukwaani na kuimba sambamba na wanamuziki wakongwe ili pia kuweza kujifunza kwa wenzao walioweza kufanikiwa katika nyanja hiyo "Huu ni wakati wa wanavyuo kukutana pamoja,kubadilishana mawazo kwa pamoja lakini pia kuna umuhimu wa wasomi kuwa na mtazamo chanya unaoendana kwa pamoja na hayo yote yatawezekana tu ikiwa watapata fursa ya kukutana kwa pamoja angalau mara chache kwa mwaka na kubadilishana mawazo alisema bwana Melleck"


Alitaja michezo itakayokuwepo siku hiyo kuwa ni pamoja na mpira wa miguu,mpira wa kikapu,mpira wa mikono,mchezo wa pool,kuvuta kamba,kukimbiza kuku,kuimba na mingine mingi itakayowafanya wote watakaoshiriki wasijisikie kuchoka.


Akitaja baadhi ya vyuo shiriki alisema ni pamoja na Chuo kikuu cha Dar es salaam,Chuo kikuu Ardhi,Chuo cha Ustawi wa Jamii,Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM)Chuo cha biashara CBE,choa cha uhasibu TIA,chuo cha kodi,Chuo cha DIT,chuo cha usafirishaji,Chuo kikuu cha Tumaini,Chuo kikuu Huria,Chuo kikuu muhimbili,Chuo cha IMTU,chuo cha Elimu DUCE,Taasisi ya uandishi wa habari na Mwasiliano ya umma SJMC, chuo cha uandishi wa habari Cha DSJ,Chuo cha habari cha TIMES,chuo cha habari Royal college of Tanzania,na chuo cha Day star vyote vya Dar es salaam.

Aidha baadhi ya viongozi wa vyuo mbalimbali walisema kimsingi vyuo vyoa vimejiandaa vyema katika kushiriki na kuishukuru Grand Malt na Mratibu kwa kuweza kuandaa tamasha hilo ambalo litakuwa kichecheo kikubwa kwa wanavyuo na nyanja ya elimu kiujumla.

Walisema kimsingi wanavyuo watatumia nafasi hiyo vizuri kwa kufahamiana na kufurahi kwa pamoja kwa kushiriki kwenye michezo mbalimbali iliyoandaliwa lakini pia ni fursa nzuri ya kukaribisha wanavyuo wanaoanza mwaka wa kwanza vyuoni kwa hivi sasa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...