Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, November 4, 2010

MASENETA MSONDO KUKUTANA KESHO


MASENETA wa bendi kongwe nchini ya Msondo Ngoma Music, wanatarajia kukutana kesho Novemba 5 katika ukumbi wa Amana, kwa ajili ya kujadi ri namna watakavyoweza kuwanasa waimbaji wawili watakaoiongezea nguvu bendi hiyo ambayo kwa sasa haina nguvu kama ilivyokuwa miaka ya nyumba.

Akizungumza na blog hii jijini Dar es Salaam Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D', alisema wamepanga kuongeza nguvu zaidi katika bendi yao ambapo sasa wanakutana ili kujua waimbaji hao watatoka katika bendi gani za hapa nchini.

Alisema kikubwa kinachowakutanisha ni kujadili majina ambayo tayari yamekwisha pendekezwa ili kujua ni msanii gani ambaye ataweza kuingia na kushika nafasi gani ambapo katika majina hayo alikataa kutaja ni waimbaji gani waliopedekezwa na kutoa katika bendi gani.

"Bado ni mapema sana kutaja ni waimbaji gani ambao tunawajadili, lakini wadau wetu na mashabiki wasubili ili tuweze kuamua nani ataingia na kutoka bendi gani hivyo kutaja sasa itakuwa vibaya kwa sababu hata mimi mwenyewe sijui ni nani atakaye kubalika," alisema.

Aliongeza kuwa mashabiki wao wasiwe na wasiwasi juu ya hilo maana wamepanga kuchukua vifaa ambavyo vitaweza kuirudisha Msondo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma pindi ilivyokuwa na muimbaji wake mashuhuri ambaye sasa ni marehema, Moshi William 'TX'.

Alisema Msondo imekuwa ikipoteza mashabiki wake kila siku hivyo hatua waliyoichukua itasaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kupata mashabiki wengi zaidi, ambapo sasa wamejipanga upya kwa ajili ya kutoa burudan kila mkoa ili kurudisha heshima iliyokuwepo.

"Sasa tumejipaga kutoa burudan ya nguvu kwa mashabiki wetu wa mkoani ambao kwa miaka mingi tulikuwa hapa hapa jijini mbali na hilo pia tutatumia nafasi hiyo kuwatambulisha waimbaji wetu wapya watakao patikana ili tuwenao sambamba," alisema.

Kwa sasa wamejipanga kutoa burudan katika ukumbi wa Meeda pub kwa kuanzia kesho tutapiga kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo hivyo kuwataka wapenzi wake waende kuiona bendi hiyo ikiwa sinza kwa wajanja pia jumamosi watakuwa Tcc Chang'gombe na Jumapili watakuwa Max bar Ilala Bungoni

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...