Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, November 27, 2010

KOCHA WA NGUMI AKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO


MDAU WA MICHEZO AMKABIDHI VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI KOCHA RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KWA AJILI YA KUENDELEZA MCHEZO HUO KWA VIJANA WASIO NA VILABU NCHINI.


Kampuni ya IRO & STEEL LTD, ALTAF& CO.PK inayojishughurisha na utengenezaji wa vyuma leo imemkabidhi kocha na mdau maarufu wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' vifaa michezo vyenye thamani ya laki tatu na hushee kwa ajili ya kuuendeleza mchezo wa ngumi.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo wakati wa hafla hiyo, Mdau binafsi na Engeneer wa kampuni hiyo, Zulfiqal Ali alisema wameamua kutoa vifaa hivyo ili kuuendeleza mchezo wa ngumi kwa vijana hasa wa kujitegemea na kuunga mkono jitihada za Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza michezo. .

Vifaa hivyo ni Groves pea nane, fulana mia sita za kufanyia mazoezi , pamoja na kamba nne za kuruka wakati wa kufanya mazoezi

Alisema kutokana na idadi kubwa ya vijana kupenda mchezo huo na kukabiliwa na tatizo la vifaa, mdau huyo ameona aweze kumsaidia kwa kumpatia vifaa kocha huyo ambaye anatoa mafunzo kwa mabondia wa kujitegemea katika ufukwe wa Coco Beach siku za Jumamosi na Jumapili.


"Baada ya kuwa nimeona juhudi za Mhamila 'Super D' ambaye siku za nyuma alikuwa bondia hapa nchini na alizichezea timu mbalimbali nimeamua kumwongezea nguvu ili aweze kufanya kazi hii kwa mafanikio lakini pia hapa tunaunga mkono juhudi za Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete katika kuthamini na kuendeleza mchezo hapa nchini,." alisema Zulfiqal.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...