Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 8, 2010

MKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM ADONDOKA NA KUFARIKI HAPO HAPO


MKAZI wa Upanga Bw.Mayuri Tradhudas anayekadiliwa kuwa na miaka 60 amekufa baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tatu hadi chini katika jengo la New Read Cross Bulding

Kwamujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mfnyakazi mwenzake na hakutaka kutaja jina lake,alisema tukio hilo lilitokea jana saa 5 asubuhi katika jengo hilo lililopo katika makutano ya barabara ya morogoro na Bibi titi.

Alisema ilipofika muda huo aliwaaga kuwa anakwenda sokoni na gafla walishangaa kuja kuona mwenzao huyo amedondoka.

"Tulikuwa wote ofisini asubuhi na ilipofika muda huo alituaga kuwa wanakwenda sokoni lakini gafla tunakuja kuitwa na kukuta tukio hili"alisema

Inadaiwa kuwa kuwa marehemu huwa ana kawaida ya kwenda sokoni kila inapofika saa 5 kwa ajili ya kwenda kununua mahitaji ya nyumbani kwake na kabla ya tukio hiolo aliaga kuwa anakwenda sokoni.

Kwamujibu wa Kamnda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala Bw.Faustine shilogile alisema muhindi huyo ni mhasibu wa Kampuni ya PS Patel & co na amejirusha mwenyewe kwa lengo la kujiua kutokana na ujumbe aliouacha
.

Kamanda shilogile alisema ,marehemu ameacha ujumbe ulioanza kwa kuandika majinayanayosemekana kuwa ya nduguzake na uliosomeka 'tafadhari nisameheni kwa kufanya msivyotaraji,muwatunnze watoto wangu Patgon and Jahuvi' .

Anasema kuwa katika ujumbe huo pia aliambatanisha namba za ndugu zake ambo wanaishi nchini Kanada huku ukisisistiza kuwa asilaumiwe mtu kutokana na kifo chake.

"Huyu mhindi kutokana na ujumbe aliouacha ni kwamba amejiua mwenyewe kutoka gorofa ya tatu na kufa na amesisistia asilaumiwe mtu kutokana na kifo chake"alisema Kamanda Shilogile.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...