Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, February 17, 2013

SIMBA YAAMBULIA KICHAPO CHA BAO 1-0 DHIDI YA BECREATIVO LIBOLO YA ANGOLA. Wachezaji wa Libolo, wakishangilia baada ya kutupia bao lao katika dakika ya 24, kipindi cha kwanza.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika, Simba, leo wamechapwa bao 1-0, dhidi ya Recreativo Libolo ya Angola.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Simba walibanwa na wageni na kuruhusu bao pekee katika mchezo huo lililofungwa dakika ya 24 na Joao Martins kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Carlos Almeida.
Simba ambao walianza mchezo kwa hofu huku wakiwaacha wageni kuutawala, ambapo dakika ya saba wanaonana vizuri na Sidnei Mariano alipiga shuti kali lililogongwa mwamba wa goli la Simba na kurudi uwanjani.
Dakika ya 13, Simba walipata nafasi nzuri ya kufunga bao, lakini mpira wa krosi uliopigwa na Nassor Chollo unakosa mmaliziaji na kuwapa nafasi mabeki wa Libolo kuondosha hatari langoni kwao.
Libolo wakicheza kwa kujiamini, akili na nguvu waliwadhibiti vizuri washambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa na Haruna Moshi ‘Boban’, ambao walikuwa wakipelekwa pembeni mara kwa mara.
Dakika moja kabla ya mapumziko, kipa wa Simba, Juma Kaseja, alifanya kazi kubwa ya kuokoa shuti kali la Carlos Almeida lililokuwa likielekea wavuni.Simba walikosa bao la kusawazisha dakika ya 64, baada ya Boban, kushindwa kutumia vizuri pasi iliyotoka kwa Haruna Chanongo, wakati tayari mpira ukiwa umewapita mabeki wa Libolo.Beki aliyerejeshwa kundini Simba, Juma Nyosso, alijaribu kwenda mbele na kufanya shambulizi la nguvu, lakini shuti lake la mguu wa kushoto lilipaa juu ya lango la wapinzani wao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...