Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, February 26, 2013

SASA NI ZAMU YA FREDERICK LAWSON NA ISSAC SOWAH KUONYESHANA UBABE.


Bondia Joseph Agbeko baada ya moja ya ushindi wake
RAIA wa Ghana Frederick Lawson na Issac Sowah wanatarajia kupanda ulingoni tarehe 8 Machi kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG)  katika uzito wa Welterwweight kwenye uwanja wa Accra Sports jijini Accra, Ghana. Mabondia hao wamepangwa katika kapambanoi ya utangukizi wakati wa mpambano mkubwa wa kugombea mkanda wa dunia kati ya bondia wa Ghana na ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa IBF katika uzito wa bantam Joseph Abgbeko na bondia Luis Melendez kutoka nchi ya Columbia iliyoko bara la Amerika ya Kusini.

Wawili hao wanatoka katika maskani ya Bukom iliyoko kwenye kiunga cha Lebanon jijini Accra kinachosifika kwa kutoa mabingwa wengi wa dunia. Kuingia kwa mabondia hawa wawili kwenye mpambano huo kutatoa burdani ya aina yake kwa mashabiki wa ngumi wa Ghana pamoja na nchi nyingi za Afrika ya Magharibi. IBF inaipa pongezi sana nchi ya Ghana iliyokuwa inaitwa Pwani ya Dhahabu au Gold Coast kwa kuonyesha nia thabiti ya kuinua vipaji vya mchezo wa ngumi na kuufanya mchezo huu kurudi nyumbani.  Ghana inasikfika sana kwa kuweza kutoa mabingwa wengi wa nguni wa zamani ambao walisifika sana kwa uwezo wao wa kurusha masumbi wakiwamo D.K. Poison, Marvelous Nana Yaw Konadu, Azumah Nelson, Ike "Bazooka" Quartey, Alfred "Cobra" Kotey na Joseph King Kong Agbeko ambaye anatarajia kuonyesha makeke yake siku hiyo ya tarehe 8 Machi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...