Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 20, 2013

TANGAZO, KWA MABLOGGER WANAOIBA KAZI ZA WATU


Uongozi wa mtandao wa sufiani mafoto blog umesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wamiliki wa blogs, kuwa wakiiba kazi za watu katika blogs mbalimbali yaani ‘Kukopi na Kupaste’ kutoka katika blog Fulani na kuweka katika Blogs zao bila kujali haki miliki ya kazi ya mtu, wala kumpa haki yule aliyechukuliwa kazi yake kwa kuandika mahala ilipochukuliwa kazi hiyo.

Kama inavyojulikana utafutaji wa habari si lelemama na ikumbukwe ili kupata habari iliyo bora na itakayowafurahisha wasomaji wako, kwenda na wakati ni lazima uihangaikie na katika kuihangaikia kuna gharama kibao zinazotumika, ikiwa ni pamoja na usafiri, pesa, na hata mafuta ya gari kutoka mahala Fulani kwenda sehemu nyingine, gharama za simu na hata kuwalipa wale unaowatuma ili kukufanyia kazi hiyo.

Kama umeweza kufanya mambo yote hayo kwa gharama unazozijua wewe uliyeweka stori, ama picha katika Blog yako, halafu watu wenye Blog Fulani wasio na uwezo wa kufanya kazi na kuchukua kazi yako kana kwamba ameokota tu jalalani na anaweka kwake ili wasomaji wake wasome, bila kuwajulisha kuwa kazi hiyo iliyomvutia imefanywa na mtandao Fulani kwa kweli inaumiza, inaudhi na inarudisha nyuma malengo hasa ya kuwa na mitandao hii, wote tutajaonekana wapuuzi.

Mtandao huu umewavumilia watu hawa kiasi cha kutosha lakini sasa imezidi kukithiri, kwani jamaa hawa wapo katika ukurasa wako kukusubiri kuona tu ulichoweka kwa wakati huo, ili wao wakopi na kupaste kwao, halafu tayari wamemaliza wala hawataki kujihangaisha kufanya kazi ili kuboresha mitandao yao na kuwavutia wasomaji wao.

‘Unapoamua kutangaza vita ujue tayari umeshajipanga kukabiliana na kila litakalotokea mbele yako, na pia umejipanga katika kutoka upinzani wa kweli ili watu waone na wakutambue, lakini sio kwa staili hii ya kuomba mtangaziwe blog zenu kupitia kwa wale walioanza mapema halafu kumbe kazi yenyewe ni kuchukua kazi za watu tu na si kufanya kazi’ yaani kukopi na kupaste,

Kuna msanii mmoja alichoshwa na wenzake wanaotamani kuingia kwenye gemu, lakini wanashindwa kuumiza vichwa kubuni ili kuweza kupata radha tofauti, na kuamua kuwafikishia ujumbe kwa kuwaimba kuwa ‘Si lazima wote tuimbe kuna michezo mingi hata kucheza bao kama huwezi kuimba, ikiwa kila wimbo unaotoka mpya umekopiwa, kama si mashahiri, basi ni Beat,

Na hata katika mablogger si lazima wote tuwe na Mablogger, kama huwezi kuumiza kichwa utoke vipi, basi kaa pembeni waachie wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, kukopi na kupaste hadi mitandao yote inakuwa sawa nini maana ya habari za haraka mtandaoni?,

Huoni kuwa mnawachosha wasomaji wenu, kwa kusoma habari na picha zinazofafa kwa wakati mmoja na katika mitandao yote?,

Tena msomaji wako wakiwa ni waelewa hawawezi kusoma tena mtandao wako kwani habari kama hiyo hiyo walikwishaiona katika mtandao Fulani muda mchache uliopita na dakika chache baadaye wanaikuta vile vile walivyoisoma kwingine ikiwa katika ukurasa wako, mara moja mara mbili msomaji huyo si umempoteza?’’.

Mablogger acheni uvivu na mjitume msisubiri kukopi na kupaste tu, na kama ukifanya hivyo basi jitahidi kumpa credit yule uliyemchukulia kazi yake.

VITU muhimu vy kuwa navyo ili kufanikisha kazi yako ya Blog, ni Laptop ‘Kompyuta mpakato’, ama Desk Top, Modem ‘Internet Wireless’, Kamera hata ndogo tu ya mkononi, na pia ujue maana ya kuanzisha hiyo Blog yako na malengo yako kwa jamii, kwani sidhani kama unaweza kuanzisha blog ili uwe ukisoma mwenyewe na naniliu wako tu.

Na kuwa na kamera si bora tu kuwa na kamera pia ujue kuitumia ipasavyo ili kunasa picha nzuri uitakayo na itakayofikisha ujumbe kwa wasomaji wako hata kwa kuiangalia tu, kwa kile ulichokusudia kuwaarifu wasomaji wako.

Baadhi ya Blogs zenye tabia ya kukopi na kupaste orodha yake tayari tunayo na baada ya tangazo hili, zikiendelea tutaziweka hewani ili wasomaji wajue ni Blog ipi ya kweli na ipi ni mamluki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...