Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 27, 2013

WATOTO WA NKRUMAH ISSAH SAMIR NA PHILIP KOTEY KUPANDA ULINGONI MACHI 30 KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA UZITO WA MIDDLE



Philip Koyey akichapa makonde na bondia Kelly Brook wa Uingereza.

Nchi ya Ghana iko katika hekaheka za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey.

Mabondia wawili hao ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na barani Afrika kwa ujumla, ambao watakutana wakati wanapogombea mkanda wa IBF AMEPG uzito wa middle.
Muziki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye 'muziki wa masumbwi' ulingoni wakati mabondia hao watakapokuwa wakionyeshana umwamba na kuwadhihirishia mashabiki wa masumbwi katika bara la Afrika kuwa wanasifa hizo kama wanavyotambulika.
Pambano hilo linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyakula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Makamu wa Rais wa IBF Africa idara ya fedha.
Kwa maana hiyo miamba hiyo inatarajia kukutana na kupanda jukwaani Machi 30,katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah.   
Nchi ya Ghana imetokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa wa ngumi kwa miaka kadhaa na kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kufuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...