Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, February 17, 2013

Tawi la Yanga Green Stone lapewa viti na Mchumi wa CCM
Yusuphed Mhandeni kulia akikabidhi viti kwa wana Yanga.
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MCHUMI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Makumbusho, Yusuph Shaban (Mhandeni), ameendelea kuwa kwenye Ilani ya chama chake kwa kuwasaidia viti 10 vijana walioanzisha tawi la Yanga, linalojulikana kama Green Stone, lenye maskani yake Mwananyamala Mwinjuma, jijini Dar es Salaam, karibu na ofisi za CCM.
Asante sana mdau wa michezo.
Kupeleka viti hivyo ni sehemu ya kuwaunganisha vijana zaidi katika suala zima la michezo, huku wakiamua kuanzisha tawi hilo kwa ajili ya kubadilishana mawazo pamoja na kuwa na mipango kabambe ya kujiletea maendeleo siku za usoni.
Akizungumza jana katika makabidhiano hayo, Shaban maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), alisema kuwa ameamua kutoa viti hivyo kwa ajili ya kuwasaidia na kuungana mkono wanamichezo walioamua kujiunganisha kwa kupitia klabu yao ya Yanga.
“Nashukuru kwa kufanikisha suala zima la viti hivi, ambapo naamini nitakuwa karibu zaidi na wanamichezo hawa bila kuangalia wanatokea katika timu gani,” alisema Yusuphed.
Naye Mwenyekiti wa tawi hilo la Green Stone, Lomole Matovolwa, maarufu kama (Big) anayevuma pia katika tasnia ya filamu, alisema kitendo cha Yusuphed kuwaunga mkono kinawafanya waamini kuwa tawi lao litakuwa imara na lenye mipango ya aina yake.
“Hapo baadaye tawi letu litafanya mambo mengi ya kimaendeleo ikiwamo wanachama wake wanaotoka hapa kufanya biashara, huku tukiamini kuwa wadau tutakuwa nao sambamba,” alisema.
Mbali na Big kuwa mwenyekiti, Katibu wake ni Ally Regani, wakati mlezi wao ni Abdul Sengwila aliyepania kushirikiana na wanachama wa wote kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya Yanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...