Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 20, 2013

WABUNGE WAIRARUA NMB KWA GOLI 1 KWA 0 WAKATI WA MCHEZO WA KIRAFIKI ULIOFANYIKA MKOANI DODOMA MWISHONI MWA WIKI


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mhe. George Mkuchika ambae alikua ndiye mgeni rasmi akikagua kikosi cha timu ya NMB  kabla ya mpambano huo.
 
Hiki ndicho kikosi kamili cha timu ya benki ya NMB kilichong’ara siku hiyo katika kutimua kivumbi kwenye uwanja wa jamhuri.

Kikosi Cha Timu ya Wabunge kilichowatoa Jasho wachezaji wa NMB na Kuwafunga goli 1 kwa 0 katika mchezo wa Kirafiki uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma
Baadhi ya wachezaji wa akiba wa timu ya NMB pamoja na mashabiki wao wakijadiliana jambo wakati wa mechi ya kirafiki kati ya NMB na Wabunge, Mchezo uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma
 Naibu waziri wa habari Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Amos Makalla (Jezi ya njano na Bluu) akipigwa chenga na  Afisa mkuu wa fedha NMB  Waziri  Waziri katika mtanange huo uliokuwa wa kukata na shoka.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azan ambae ndiye mlinda mlango wa timu ya wabunge  (Jezi  ya rangi ya chungwa) akiongoza wanatimu kufurahia goli moja walilolipata na kuwapa ushindi dhidi ya timu ya NMB

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...