Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 18, 2013

TENISI KUCHAGUANA JUNI 22Na Elizabeth John
WAKATI zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kugombea uongozi wa Chama Cha Tenisi Tanzania (TTA), lilifika tamati tarehe Juni 17, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Denis Makoi amechukua fomu ya kutetea kiti hicho.

Wagombea 14 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho na ucahaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Juni 22 jijini Dar es Salaaam.


Kwa mujibu wa Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, wagombea wengine waliochukua fomu ni Mtangazaji wa Magic FM, Fina Mango na Mathisut Sele Mbajo ambao pia wanawania Uwenyekiti wa chama hicho.


Alisema wagombea wengine waliojitokeza kuchukua fomu ni Joyce Marwa akiitaka nafasi ya Uhasibu, William Kallaghe aliyejitosa ukatibu mkuu, Josima Mutale anawania ukatibu msaidizi huku wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kiango Kipingu, Swalehe Malimbo, Gilbert  Peter, Majaliwa Majuto, Nico Jonas, Morris Loje na Ismail Ngulingo.


“Zoezi hili limeenda salama, mimi nawasisitiza tu wadau mchezo huu wawachague viongozi ambao wanaamini watawapa ishirikiano wa kutosha                      katika kipindi chake cha uongozi, siku ya usaili kwa wagombea hao itatangazwa mapema kabla ya siku ya uchaguzi,” alisema Chacha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...