Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 29, 2013

WALTER AISAMBAZA 'DORODORO'Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Siachi’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Walter Chilambo ameachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Dorodoro’.

Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Walter alisema kazi hiyo kaisambaza hivi karibuni na anaomba mashabiki wake waipokee kwa mikono miwili.

“Naimani kazi hii itafanya vizuri katika tasnia hiyo kwani mashairi yaliyopo ndani yake yamesimama na yanaujumbe kwa jamii,” alisema msanii huyo ambaye ni mshindi wa Bongo Star Search mwaka jana.

Akizungumzia uandaaji wa video ya kazi hiyo pamoja na ile ya ‘Siachi’ kwamb ayupo katika hatua za mwisho na anawaomba mashabiki wake wasichoke kumsubiri.


“Nitatangulia kutoa video ya ‘Siachi’ naimani itakua nzuri kutokan ana maandalizi ya muda mrefu, najua mashabiki wanaisubiri kwa hamu ila nawahaidi ipo karibuni wataiona,” alisema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...