Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 18, 2013

FOMU ZA UONGOZI BFT ZADODA
Na Elizabeth John
WADAU wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) wameshauriwa kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi wa chama hicho baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao.

Hadi jana hakuna mgombea aliyejitokeza kuchua fomu za ugombea katika chama hicho ambapo zilianza kutolewa Juni 4 mwaka huu katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Michezo wa BMT, Benson Chacha alisema hadi jana hakuna mwanachama yeyote aliyejitokeza kuchukua wala kuulizia fomu za kuwania uongozi katika chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Julai 7 jijini Mwanza . 

Alisema usaili kwa wagombea ambao watajitokeza kuwania nafasi za uongozi utafanyika Julai 5 kabla ya kuanza kwa taratibu za uchaguzi wa chama hicho ambapo wanachama na wadau mbalimbali watashiriki uchaguzi huo.

“Nawaomba wadau wajitokeze kuwania nafasi za uongozi pamoja na kushiriki uchaguzi ili baadae wasije kulalamika maana hii ni fursa pekee kwao wanapaswa kuitumia,” alisema Chacha.

Fomu zinazotolewa ni kwa nafasi ya Rais, Makamu, Katibu Mkuu, Mweka Hazina na wajumbe tisa na gharama za fomu hizo kwa  nafasi ya Rais sh 150,000, Makamu, Katibu Mkuu, Mweka Hazina ni sh 100,000 na 50,000 kwa wajumbe.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...