Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 29, 2013

SIMULIZI ZA MZEE MADIBA ;MANDELA BONDIA ALIPOKUTANA NA BONDIA


2 1bd4f
Ndugu zangu,
Kuna simulizi nyingi za Mzee wetu Madiba. Hakika, Nelson Mandela hajawahi kuwa mpenda makuu.
Mzee Mandela yuko simple sana, ni tangu enzi za ujana wake. Lakini, kuna ambao hawajui kuwa Mandela anapenda sana mchezo wa ngumi, na kuwa , yeye mwenyewe aliwahi kuwa bondia.
Kuna wakati akiwa Ikulu kama Rais, Mandela alipata habari za bondia wa Afrika Kusini aliyetwaa taji la  kimataifa. Mandela alifurahishwa sana na habari hizo. Akataka ampongeze mwenyewe bondia  huyo.
Siku moja akiwa na wasaidizi wachache sana, Mandela alikwenda hadi nyumbani kwa bondia huyo. 
Alihakikisha kuwa
bundia huyo yuko nyumbani kwake. Alipofika, Mandela aliwaambia wasaidizi wake wakamwambie bondia huyo kuwa nje kuna mtu anayehoji ubingwa wake. 
 Wamwambie kuwa  mtu huyo ( Nelson Mandela) anadai kuwa yeye ndiye bingwa wa uzito huo katika Afrika Kusini ( Nelson Mandela!) Kwamba anataka mkutane mpange siku ya kupigana ili apatikane mshindi halali wa taji hilo.
Basi, bondia yule akapokea habari hizo na akatamani sana amwone huyo anayedai kuwa ana ubavu wa kupambana naye.
Alipotoka nje akakutana na Nelson Mandela akiwa amesimama getini na amekunja ngumi yake. Akatania; “ Nimekuja kwako tuzipige ili dunia imjue bingwa halisi!”
Ikawa ni furaha kubwa kwa bondia yule. Hakuamini macho yake. Kuwa Rais wan chi amekuja nyumbani kwake kumpongeza.  Kumpongeza kwa jambo kubwa alilolifanya kwa taifa la Afrika Kusini. 
Na Mandela akawa tayari kuingia nyumbani kwa bondia huyo na kunywa nae chai!
What a Great Leader Of Africa! Yes, Nelson Mandela!
Maggid Mjengwa,
Iringa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...