Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 27, 2013

MAKAMU WA RAIS DK.MOHAMMED GHARIBU BILAL AFUNGA MAFUNZO YA MAOFISA NA WAKAGUZI WASAIDIZI WA JESHI LA POLISI


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emanuel
Nchimbi (wa nne kushoto), akiwa na viongozi
mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama katika
hafla ya kufunga mafunzo ya maofisa na wakaguzi
wa Jeshi la Polisi iliyofanyika viwanja vya Chuo cha
Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia),
akimvika cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), J
ohn Makuli (katikati), baada ya kufuzu mafunzo hayo.
Maofisa 295 walifuzu mafunzo hayo na kutunukiwa
vyeo vya wakaguzi na maofisa. Makamu wa Rais
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo.
 Wageni waalikwa na ndugu za maofisa waliofuzu
mafunzo hayo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Gwaride maalumu la maofisa hao likipita mbele ya
mgeni rasmi  Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib
Bilal kwa mwendo wa haraka kwenye hafla ya kufunga
mafunzo ya maofisa na wakaguzi wa Jeshi la Polisi
iliyofanyika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya
Polisi Kurasini Dar es Salaam leo.

 Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakionesha
jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
 Maofisa wa Polisi wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Askari wa Kikosi cha Farasi wakipita katika uwanja
wa paredi wakati wa hafla hiyo
 Wahitimu hao wakiwa uwanja wa paredi. (Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com)
 Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharibu Bilal akitoka
kukagua gwaride la maofisa hao waliohitimu mafunzo
ya uofisa na ukaguzi.

 Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharibu Bilal,
akimvika cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi
Alikunda Urio.
 Waziri wa M,ambo ya Ndani ya Nchi, DK. Emanuel 
Nchimbi (katikati), akiteta jambo na Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Hassan Ndomba (kulia). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema.
 Gwaride maalumu la maofisa hao likipita mbele ya
mgeni rasmi 
 Wahitimu hao wakila kiapo cha utii.
 Maofisa wa Polisi wakionesha utalaamu wa kucheza
mchezo wa karate wakati wakikabiliana na adui.
 Mmoja wa askari wa mwanamke wa jeshi hilo (kulia),
akionesha namna ya kukabiliana na adui.
 Askari hao wakionesha namna ya kukabiliana na adui kwa kutumia mikono.
 Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakionesha
jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakionesha
namna ya kukabiliana na wananchi wakati wa vurugu.

Na Dotto Mwaibale

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Dk. Mohammed Gharibu Bilal amesema serikali haitakuwa tayari kuvunja kiapo chake na kuona amani ya nchi natoweka.

Kauli hiyo aliitoa wakati akifunga mafunzo ya Uofisa na Wakaguzi Wasaidizi kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini Dar es Salaam leo.

"Serikali haikotayari kuona amani ya nchi ikivurugwa kupitia kundi la aina fulani hivyo ninyi polisi ndio wenye wajibu wa kulinda amani hiyo pamoja na watu na mali zao" alisema Bilal.
 
 Dk.Ghalib Bilal ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo hayo alisema hivi sasa nchi yetu imekuwa ikikabiliwa na matukio ya vurugu zinazotokana na vyanzo mbalimbali.
 
Alisema baadhi ya vurugu hizo zinasababshwa na hisia za kiimani,kisiasa na kijiografia ambazo madhara yake ni makubwa na tayari yameathiri wananchi wengi.
 
"Wananchi wa Tanzania hawapendi kabisa kuona nchi hii ikigeuka kuwa ukanda wa vurugu, tena sisi kama Taifa hatuwezi kunifaika na vurugu zisizoisha"alisema Dk.Bilal
 
Alisema  jeshi la polisi lilihapa na kusimamia amani na utulivu nchini hivyo tunaamini kuwa amani hiyo italindwa kutokana na viapo walivyoapa.
 
Aliongeza kuwa hivi karibuni kumeibuka baadhi ya wananchi kwa sababu zao wameanza kubeza na kudharau kazi wanazofanya askari wetu kibaya zaidi watu hawa wanaota siku moja watashika dola ya nchi yetu ili waiongoze nchi.
 
"Siamini macho yangu kama ndoto zao zitatimia kama wataendelea na tabia hii ya kudharau na kutoeshimu mamlaka tulizojiwekea wenyewe kwani kazi ya askari si sawa na kufanya siasa kwani kazi ngumu lakini ni muhimu kuliwekea Taifa katika twasira ya maendeleo"alisema Bilali.
 
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.Emanuel Nchimbi amesema askari wa tano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa makosa ya kuiba nyaraka mbalimbali za serikali na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha baada ya kufungua akaunti kwa kutumia jina la jeshi hilo.
 
Alisema watu hao tayari wameshakamatwa na muda wowote watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao kwa kuwa tayari jalada lao limeshapelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali.
 
Nchimbi alisema kutokana na tuhuma hizo kujitokeza aliamua kuunda tume ya uchunguzi ili kugundua ni nani anayefanya tuhuma hizo, tume hiyo ilikuwa inaongozwa na Kamishna Msaidizi wa polisi Advocate Nyombi kutoka makao makuu ya upepelezi ya makosa ya jinai.
 
"Sikutaka kufumbia macho suala hilo timu hiyo ilifanya kazi yake na juni 22 mwaka huu ilitoa majibu na kubaini askari wa zimamoto wenyewe ndio wanahusika na ubadhilifu ndani ya jeshi la zimamoto nchini"alisema Nchimbi.
 
Aliwataja watuhumiwa wanaotuhumiwa kuwa ni Mkaguzi Msaidizi wa zimamoto Joseph Mwasabeja, Koplo wa zima moto Hashimu Kapamba, Koplo wa zimamoto Boniface Mbele,Sajini Meja wa Zimamoto Dankan Mwakajinga na Koplo wa Zimamoto Kenned Kipali ambao wanatoka ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na nje ya mkoa.
 
Hata hivyo Waziri Nchimbi alisema vitu walivyopatikana navyo ni pamoja na hati ya akaunti ya benki inayotumika kuibia serikali,mikanda 82 ya askari wa jeshi la zimamoto na stakabadhi mbalimbali za malipo zinazotumiwa na jeshi hilo.
 
Aidha, alisema mtuhumiwa Kapamba alikamatwa na na stakabadhi za malipo ya serikali (ERVs)ambazo ni za kughushi hati na fomu mbalimbali za jeshi hilo zinatumika katika ukaguzi wa viwanda na majengo.
 
Vilevile alisema kuwa kati ya watuhumiwa hao mtuhumiwa mmoja ni mtoto wa Kamishina wa pwani,ambaye aliwasiliana naye na kumtaka amwasilishe mtoto wake ndani ya masaa mawili kwa ajili ya kujieleza dhidi ya tuhuma hizo.
 
Hivyo aliwataka maofisa hao wajue kuwa wanakazi kubwa wanapokwenda kazini na aliwataka wananchi wote watimize wajibu wao kwa kufuata sheria za nchi na kujiepusha na vitendo vya namna hii ambavyo vinavunja heshima yao na jeshi la zimamoto.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...