Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 25, 2013

NMB YAFADHILI UMITASHUMTA MANISPAA YA SUMBAWANGA


Benki ya NMB imefadhili UMITASHUMTA kwenye manispaa ya Sumbawanga kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni tisa. Lengo kuu la ufadhili huu ni kusaidiana na UMITASHUMTA katika kuibua na kuendeleza  vipaji vya michezo kwa shule za msingi nchini Tanzania.
 Meneja wa NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku akimkabidhi  Ofisa Elimu, Modesta Zambi  sehemu ya vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye UMITASHUMTA  manispaa ya Sumbawanga. Makabidhiano haya yalifanyika hivi karibuni kwenye manispaa hiyo.
Maofisa wa Benki  ya NMB  na maofisa wa Manispaa ya Sumbawanga wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB  Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (tatu kulia)  mara baada ya kukabidhi vifaa vya michezo.
 Mipira iliyokabidhiwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...