Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 27, 2013

RAIS WA SRI LANKA MANIDA RAJAPAKSA AWASILI NCHINI LEORais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi.
Mtoto Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete akishuhudia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...