Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 21, 2013

FILAMU YAMFANYA IRENE PAUL AJIFUNZE KUENDESHA BAJAJI

Na Elizabeth John

AKIWA bado anafanya vizuri katika filamu, mwanadada  Irene Paul amesema kwamba filamu ya kibajaji  ilimfanya ajifunze kuendesha chombo hicho kwa lazima ili kuleta uhalisia.

Japo awali alisema aliona kama ingekuwa ni kazi ngumu sana kwake lakini ilimbidi kukaza roho kwa kuwa yeye ni msanii ambaye angependa kuwaonesha mashabiki wake vitu vya ukweli na si vya kuongopea.


Katika filamu hiyo ambayo safu hii iliichambua wiki iliyopita, Irene ameweza kuitendea haki akiwa sambamba na mchekeshaji Salum Haji’Mboto’ ambapo kumejaa vituko vitakavyokufanya ucheke hata  kama umemka vibaya siku hiyo.

Mwanadada huyo ni kati ya wasanii ambao wanakuja juu katika tasnia hiyo ambapo mwaka huu amefanikiwa kuchukua tuzo ya msanii bora wa kike anayechipukia, zilizotolewa katika ukumbi wa Ubungo Plaza wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...