Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 26, 2013

Yusuph Mlela aibukia kwa Miss Serena

Yusuph Mlela aibukia kwa Miss Serena

Yusuph Mlela katika pozi
 MSANII mahiri wa filamu nchini, Yusuph Mlela 'Angelo' anajiandaa kuingiza sokoni filamu yake mpya iitwayo 'Miss Serena' ambayo ameifyatua chini ya kampuni yake binafsi iitwayo 'Mlela Films Production'.
Akizungumza na MICHARAZO, Mlela alisema filamu hiyoi aliyoigiza na wakali wenzake kama Salma Jabu 'Nisha' , Sabrina Rupia 'Cathy' na Seleman Abdallah 'Barafu' ipo katika maandalizi ya kuwachiwa wakati wowote kuanzia sasa.
Mlela alisema filamu hiyo ya kimapenzi na yenye mafunzo kwa jamii ni ya tatu kuzalishwa na kampuni yake tangu alipoianzisha hivi karibu kama njia ya kujikomboa.
"Kaka nimekamilisha filamu yangu mpya ambayo ni ya tatu kuzalishwa na kampuni yangu na itafahamika kwa jina la 'Miss Serena' ambapo imewashirikisha wakali kadhaa nikiwemo mimi mwenyewe, Nisha, Barafu na Cathy wa Kaole," alisema Mlela.
Mlela aliyetambulishwa kwenye ulimwengu wa filamu mwaka 2006 kupitia filamu ya 'Diversion of Love' kabla ya kujipatia umaarufu katika filamu zaidi ya 30 alizocheza mpaka sasa alisema kazi hiyo mpya ni moja ya kazi nzuri alizozalisha baada ya kutoa Angel na Poor Minds.
Mkali huyo ambaye pia ni mwanamitindo alisema mashabiki wake wakae mkao wa kula kupata burudani kabambe wakati akiwa 'location' kwa sasa akishirikishwa kwenye kazi mpya ya Wastara Juma 'Stara'.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...