Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 22, 2013

LUCY TOMEKA ANYAKUA TAJI LA REDDS MISS KINONDONI 2013

 Mshindi wa Redds Miss Kinondoni 2013, Lucy Tomeka akivalishwa taji lake na mrembo aliyekuwa akilishikilia taji hilo Redds Miss Tanzania 2012/2013, Bright Alfred. Lucy Tomeka aliweza kuchukua taji hilo kwa kuweza kuwagalagaza wenzake wapatao 12 katika kinyang'anyiro hicho kilifanyika jana ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar.    
 Akivalishwa utambulisho wake.
 Showlove...
 Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora wakifurahia kwa pamoja, katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi. Wengone ni Sarah Paul (kwanza kulia) na Linda Joseph (kwanza kushoto).

  Tatu bora ni katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi.
Na Mwandishi Wetu
KUMEKUCHA! Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred ameendelea kuvua mataji yake baada ya juzi usiku kumkabidhi taji la Redd’s Miss Kinondoni,  Lucy Tomeka katika shindano lililofanyika ukumbi wahoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam.
 
Kwa sasa Brigitte, amebakiwa na taji moja tu la Redd’s Miss Tanzania baada ya kuvuliwa jingine la Redd’s Miss Sinza wiki mbili zilizopita.
 
Katika shindano hilo lililovuta hisia za watu, kulikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo 12 walioshiriki katika kinyang’anyiro hicho, kilichoambatana na burudani kibao.
 
Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni Lucy Tomeka, Prisca Clement, Phillios Lemi, Sarah Paul na Linda Joseph na hivyo kuwaweka roho juu mashabiki kutojua nani atatwaa taji.
 
Katika shindano hilo nafasi ya pili ilikwenda kwa Prisca Clement, akifuatiwa na Phillios Lemi, hivyo kutoa fursa kwa washindi hao kuingia moja kwa moja katika shindano la Redd’s Miss Tanzania.
 
Kinyang’anyro cha Redd’s Miss Tanzania kwa sasa kinadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...